Stori: Gladness Mallya
Oooh nooo! Miaka miwili baada ya kufunga pingu za maisha (ndoa) na mwanaume aitwaye Kauli Juma, imefichuka kwamba ndoa ya prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima ina shida kwani haishi na mumewe, ikidaiwa kwamba kila mmoja anaishi nchi tofauti na mwenzake.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Sauda, kilisema kwamba baada ya wawili hao kufunga ndoa, Kauli aliondoka kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ alikokuwa akifanya shughuli zake kabla ya kufunga ndoa na hadi leo hajawahi kurudi Tanzania.
“Yaani baada ya Sauda kufunga ndoa, mumewe alikaa kwa miezi michache hapa Bongo, nasikia hata tendo la ndoa walifanya mara mbili tu.
“Hata alipojifungua na mtoto kufariki dunia kwa bahati mbaya, mumewe hakuwepo na hadi leo hajarudi, ukweli inauma sana ila Sauda ni mvumilivu kwani ndoa yake ni shida,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Sauda ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli anaishi Sauzi. Tangu tukiwa wachumba tulielewana kwamba tukioana kila mtu ataendelea kuishi anapoishi hivyo mume wangu anafanya shughuli zake nchini Afrika Kusini na huwa anakuja mara mojamoja akiwa na nafasi au akiwa likizo.
“Mimi siyo mtu wa kujionesha kwamba eti mume wangu yupo nchini hivyo akija huwa ni kimyakimya anakaa tunaendelea na mambo ya familia yetu basi muda ukiisha anaondoka na tulikubaliana tangu tukiwa wachumba hivyo ikitokea mmoja wetu ameamua kumfuata mwenzake na kwenda kuishi naye hakuna shida,” alisema Sauda.
Sauda aliongeza kwamba ndoa yake iko vizuri na hawajaachana na endapo ingekuwa haipo asingevaa pete ya ndoa.
“Ndoa yangu haijavunjika, tuko vizuri na mume wangu japokuwa tuko mbali lakini kila mmoja anamwamini mwenzake,” alisema Sauda.
Wadau wanaifananisha ndoa hiyo na ya Aunt Ezekiel na kudai kuwa wawili hao hawachekani.
GPL
MAISHA HAYO NI KAWAIDA SANA NOWER DAYS, MUME TZ MKE UK
ReplyDeleteHalafu huyu jamaa mwenye mke UK nimesikia habari zake dah aisee. Mke wake anachepuka kiulainiiii haina shida na mjamaaa anachepuka vile vile na Bongo Movie hahaha
DeleteITAFIKA KIPINDI WATU WATAELEWA, KWA SASA WANAONA HAIWEZEKANI
ReplyDeleteKawaida sana hiyo na maisha yanaenda fresh...mimi na mume wangu mwaka wa kumiyeye yuko zake uk tumejipangia tu kila mwaka anakuja anakaaa cku zake kadhaa anasepa kikubwa uaminifu na kujaliana...
ReplyDeleteAu sio. Halafu akija wazee wa mjini inawabidi wale pause kwanza ili mjamaa apate vyake vya kiuhalali halafu akiishia kwenda kupiga box wazee wanaendeleza libeneke kama kawa dah haya maisha sio mchezo ni plans tu
DeleteMange and lance.mange bembeleza mume Chezea Mlo wewe
DeleteBy the way hiyo ya kukaa mbalimbali ni kitu poa sana. Inaondoa zile stress za kubanana banana. Na pia inawapa nafasi ya kufanya vyenu kwa uhakika bila ya kuwekeana mizengwe. Hata siku mkiachana inakuwa ile no hard feelings au sio. Kimya kimya tu
ReplyDeletekwa nini unawaza mabaya (kuachana ) waswahili wanasema aliwazalo mjinga .........??? mpinge shetani kwa mawe na moto wa roho mtakatifu
DeleteHaha mjipe Moyo tu.mwanaume anaefanya fanya hivyo bonge la red flag .HE IS NOT IN TO YOU .
Deletehiyo si kawaida hata kidogo ikija kutokea wakaja ishi pamoja kwa miezi au mwaka hauishi utasikia hakuna ndoa. mume Uk mke Tz wanakizi vipi haja za miili yao. Muogopeni Mungu jamani.
ReplyDeleteHata mimi nashindwa elewa kama kweli kuna uhalisia katika mambo kama hayo. Anyways let us see and wait
DeleteKwa niñi mtu ahame mji kwa ajili ya kazi makubwa
Deleteyaani ndoa za namna hiyo huwa hazina joto hasira , napenda kuziita ndoa za msimu zina raha yake jamani achaaaH
ReplyDeletenikweli mkikutana yaani mnakuwa honey moon ya nguvu
ReplyDeleteSafisana kilamtu nazake.mradi ujielewe nakujiheshimu tu.mkikutana malovee mwanzo mwisho hamuwezi kugombanasana kama wote mnajitambua nakupendana.akija toka safari michepuko yote stoop niko wife au niko na hubby back off kwa mda.hii safisana kama mnapendana kwa dhati
ReplyDeleteYaaan ni rahaje? cku akirudi full bata mnaonana wapyaaa kiubwa upendo kuthaminiana na kuheshimiana na.. na hii mitandandao yetu ya kisasa mitango mi skpy... aaa kama mko pamoja wenyewe ucku watoto wamelala tunafanya yetu kwenye cm mpaka kila mtu anaridhika na usingizi unampitia na cm yke mkonono asikwambie mtu yaan maisha yanaenda bila tabu na haswa ukimpata mwanaume anae jua mapenzi ya kwe cm? alafu mna chat mnaonana hivi...maisha yanaendaaaaa
ReplyDeleteWewe umesikia hizo habari? Kwanza mimi ndo naishi bongo mume wangu ndio yuko uk... ckatai kule stakuwa anafanya yake si mwanaume kakamilika... kikubwa nachoshukuru ni jinsi anavyonijari na mwanae na ajua umuhimu wakurudi na ni lazima arudi kila mwaka kujakufanya yetu then anaenda kurndelea na kazi zake... mbona fresh tuuuu
ReplyDeletelakini ni vizuri mkiwa pamoja kama wanandoa, sidhani kama mke/mume anaweza kuzuia hisia za kimwili kwa muda wa zaidi ya mwaka kweli, labda kama hakutani na watu au ana kazi ya kuunda Meli inayomchosha na kumpotezea hisia kabisa, lakini vinginevyo ndio tunazidi kupigana vikumbo na wake/wame za watu huku mitaani kisa tamu!
ReplyDeleteKutafta kutombewa huku... migubeli yenyewe hii mnaishi nyumba moja lakini anagawa mpopo ka pumzi je upo nchi nyengine???? Ka maisha hayajatulia bora kutooa, hv ndugu tunaijua maana ya ndoa kweli??? Au inafungwa ilimradi tu kufirahisha watu kutwa moja kama flan kaoa au kaolewa???
ReplyDelete