Ommy Dimpoz Awachanganya Kimalovee Jokate na Vanessa Mdee

Acha kabisa! Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo ni madai ya Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwachanganya kimalovee, mastaa wenzake, Jokate Mwengelo ‘Kidoti’ na Vanessa Mdee ‘Van V’ au V-Money


Chanzo makini kilisema Jokate na Vanesa kwa sasa ni kama chui na paka kufuatia hivi karibuni Jokate kudaiwa kuingilia penzi la mwanzake na mpaka sasa eti ndiye aliyeshikilia usukani.

“Sasa hivi Jokate na Ommy ni mahaba niue kwani mara nyingi wanakuwa pamoja.
“Hadi Jokate anakwenda geto kwa Ommy jambo ambalo limesababisha yeye na V-Money kutoelewana kwani awali ndiye alikuwa kiburudisho cha Ommy,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizi, mwanahabari wetu alimtafuta mhusika mkuu Ommy Dimpoz ambaye alikuwa na haya ya kusema:

Ehee! Ndiyo nasikia kwako, kwani wasanii haturuhusiwi kupendana jamani, hata Mwalimu Nyerere (Baba wa Taifa) alisema tuwe pamoja kwa hiyo Jokate ni rafiki yangu wa karibu na huyo Vanessa sijawahi kuwa na uhusiano naye but (lakini) alikuwa mshikaji tu.”

Juhudi za kuwapata Jokate na Vanessa ziligonga mwamba baada ya simu zao kuita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea ili kila mmoja aeleze la moyoni mwake.Juzikati picha za Jokate na Ommy wakiwa kimahaba zilizagaa kwenye mitandao mbalimbali hali iliyozua viulizo kibao kwa mashabiki wao.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmm.. Ni shida

    ReplyDelete
  2. Mmmm.. Ni shida

    ReplyDelete
  3. Mmmm.. Ni shida

    ReplyDelete
  4. duuu, ndio lazima ili uendelee kujulikna

    ReplyDelete
  5. i lv u jokate coz n mwnmk mwny kujua ktfut ktk maisha.il kw hl hpn shame on u jojo

    ReplyDelete
  6. i lv u jokate coz n mwnmk mwny kujua ktfut ktk maisha.il kw hl hpn shame on u jojo

    ReplyDelete
  7. i lv u jokate coz n mwnmk mwny kujua ktfut ktk maisha.il kw hl hpn shame on u jojo

    ReplyDelete
  8. sasa hiyo midomo ya jokate ndio swaga au!! hilo suala la mapenzi ni personal issue sana za mtu kwani atakaechoka nadhani ataacha, tuwaache walale

    ReplyDelete
  9. muumini jamani kafanya nini tena

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad