Sababu Zilizomfanya Dogo Janja Aache Shule, Hili Atakuja Kulijutia Baadae

Rapper kutoka Arusha, Dogo Janja ameamua kuacha shule ili kusomea masomo ya muziki. Akiongea na 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM, Janjaro amedai kuwa usumbufualiokuwa akiupata shuleni ndio sababu kubwa iliyomfanya aache shule.

“Shule ambayo mimi nimesoma nilikuwa napata matatizo kwasababu kitu kidogo ambacho mnaweza mkafanya wote lakini wewe ukaonekana chanzo. ‘Msanii mhuni, huyu hivi,” alisema rapper huyo.

“Sometimes unaweza ukawa unasoma watu wengi wako dirishani wanapita wanakuangalia. Au unaweza ukakosea.. yaani wanakuwa wewe ni mtu ambaye upo sahihi all the time. Kwa mfano labda unajua zile za kushtukizwa ‘fulani jibu swali’ kila saa unaulizwa wewe,” aliongeza.

“Kwahiyo unakuwa hakuna pale Uabdul, unakuwa unaweka Ujanjaro Udogojanja. Kwasababu unajua ile kushtukizwa kila saa unakuwa unahisi kama mwalimu anakuandama sana. Au kwenye mtihani, mnaweza mkawa mnafanya wote mtihani lakini mwalimu anakuja kukusimamia wewe, anakukazia kinoma.”

Nini mtazamo wako kuhusiana na sababu hiyo ya Dogo Janja iliyomfanya aache shule?

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ngoja afikishe 25 above atajuta joh

    ReplyDelete
  2. Walimu, na sekta ya elimu ,ifanyie kazi,haya matatizo,nchi zetu za kiafrika huwa tuna angalia ,hasara ,tu,bila kuangalia chanzo cha hasara,mwalimu angekuwa na saikologia nzuri,angemsaidia angependa shule,vipaji vingi vya vijana ,haswa afrika vinakufa kwa sababu ndogo ndogo,sana kukosa mtaji,mwalimu mzuri,mshauri,etc,tuyafanyie kazi haya ,tusibaki na lawama wangine wana acha shule kwa sababu ya snow,tatizo la rangi,au kutojua lugha sehemu nyingine za dunia,tuyafanyie kazi haya,nchi na taifa litabadilika ,mdau ma.

    ReplyDelete
  3. huu usemi wa majuto ni mjukuu atakumbuka..afu wazaz wake nao wamechangia..km baba ake anaboa yan hana ushauri mzuri kwa mwanae

    ReplyDelete
  4. Hilo toto hovyo sana wakati Madee anampandisha basi kurudi ngarenaro watu walilalama eti anamuonea sasa umeukubali ukweli,hilo kile kitu cha Arusha kaanza kukitumia akiwa mdogo sana.

    ReplyDelete
  5. anadhan ataendelea kua juu siku zote ajuta

    ReplyDelete
  6. anadhan ataendelea kua juu siku zote ajuta

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad