Stori: Shakoor Jongo na Makongoro Oging’
NIkweli kimenuka! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo kikaangoni, habari zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake, Godfrey Nzowa nao wananyanyua miguu yao kumfuatilia, Amani limesheheni.
Habari za kiintelijensia zilidai kwamba, kisa cha kikosi hicho kufanya hivyo kinadaiwa kuwa, serikali inamhofia kujihusisha na biashara hiyo haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ nje ya nchi kwa kutumia kivuli cha kwenda kufanya shoo.
Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambaye hakupenda kuchorwa jina gazetini, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu.
MAELEKEZO ALIYOPEWA
“Tumempa maelekezo Diamond, atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara nyingine.
“Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama amezipata kihalali,” alisema afisa huyo.
Afisa huyo aliendelea kusema kwamba, uchunguzi wao pia umebaini kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa akinunua nyumba kila anaporejea kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi, jambo ambalo taasisi haiamini kama kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo moja, kiasi cha kumwezesha kununua nyumba jijini Dar
GPL
Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhhh
ReplyDeleteKwa nn msifuatilie kimya kimya
ReplyDeleteNdio zao. Wanaanza kwa kutangaza lakini mwisho inakuwa kimyakimya,
Deletekama yale ya staa wa "the original comedy" yameisha kimyakimya.
sasa mmeshamwambia, unafikiri yeye mjinga hata kama nikweli alikuwa anafanya, atafanya tena? ukimshuku mtu, mpeleleze, jamani hii ndiyo itelejensia gani?
ReplyDeleteLISEMWALO LIPO,KAMA HALIPO LAJA
ReplyDeletendio maana nchi haiendelei, hawafanyi kazi kwa vitendo ni majungu tu, kwa shoo anazopiga huyu dogo sidhani kama ni kitu cha ajabu kununua nyumba, wao wameamua kukaa kwenye stuli ndefu na kusubiri warembo, mwenzao amechagua kununua nyumba wanasema ni unga, tena nafurahi Sana huyu msanii hapendi kujibujibu hoja zisizo na mashiko
ReplyDeletehizo pesa nyingi ambazo wameziona kwenye akaunti yake ni sh ngapi? usikute wameona milioni kumi ndo wanasema pesa nyingi, kama kuna bilioni moja kwenye akaunti yake hata mimi nitamshtukia!! sababu kwa manunuzi na matanuzi ya huyu dogo kuwa na hiyo hela cash imetulia kwenye akaunti dah!! tusidanganyane!! na wala siyo wivu, hii ni bongo bwana naijua, sidhani kama kuna msanii wa hapa ambaye anapiga shoo tu na kuuza nyimbo zake na kuwa mtu wa matanuzi nakufikia kuwa na bilioni moja cash kwenye akaunti imetulia na ukizingatia kuna watu wengine wako kwa ajili yakumuuibia kazi zake na kumtapeli juu!! sijui!!
ReplyDeleteWe ufuatilii interview za dai mwenyewe kasema Ana billion kwenye account,anahofia maisha yake.sikulizeni interview, mshwreee
DeleteJEALOUS zitawauwa muacheni Diamond na maendeleo yake ndio maana wa Bongo hatufiki mbali wasanii wetu tunawarejesha nyuma kwa ushamba wetu na wivu wa maendeleo ya mtu mtu mwengine Bongo noma tutakuwa nyuma maisha kwa Jealous za ki Bongo.
ReplyDeletemkiambiwa ukweli mnasema wivu, kuweni na akili za kufikiria kidogo!! muziki wetu baaaddoo haujafika hivyo mbali mpaka msanii wetu wakibongo aweze kumiliki fedha zote hizo!!! na huo ni ukweli, na siyo muziki tu, sanaa yoyote ndiyo maana wengi wanabebeshwa sembe!!! JK anajitahidi kutuendeleza lakini baaadooo tuko nyuma!!! mbaya zaidi matapeli na wezi wa hizi sanaa ndiyo chahu kubwa yakuturudisha nyuma!!! wivu ni ujinga tu!!!
ReplyDeleteRoho mbaya haijengi, Dangote anajituma simchezo. Kuna clip niliwahi kuiona akifanya show Congo, huo umati na mapokezi alopata sio ya kawaida......mwenyewe alishasema hapigi show chini ya mil. 10, na pia si'muhongaji, sasa hapo cha kushangaza kuwa na pesa hizo ni kipi? Kama kweli anafanya biashara hiyo kwa nini hamjamkamata kama akina Masogange?? NI HILO KWELI AU M'NAJINGINE.......ni shiiiiiiiiiiiider!!
ReplyDeletesasa ndio ataonyesha kipato alichopata kwa hizo shoo zake,tuone kama zinalipa kiasi cha kuweza kununua nyumba 15 Dar.si document anazo bhana!
DeleteLisemwalo lipo,waendesha bajaji zake ndio wamelipua bomu.
ReplyDeleteSema yataisha tu,hii ndio Bongo.
hehe akili nyingine fupi!!! watu tunaomba kila siku TZ ipae hata kwa lolote lile, nyie mnakimbila kwenye akili zenu zakipumbavu kwamba mtu ana roho mbaya au wivu, hata ukimwonea wivu itakusaidia nini wewe binafsi? huo ndiyo ukweli Tanzania badoo saanaa!! kubalini tu madanganyika!!
ReplyDeletesimhongaji? anoy 4:29PM hakukuambiaga kwamba alishahonga mwanamke gari la milioni kumi? au hao vimada wake unawaonaje? wamejipeleka tu eeh!!! hawapi chochote eehh!
ReplyDeleteHapo sasa!
Deletewabongo hawapendi mtu apate kitu washaanza kumfatilia muachieni waku wakamata wamejaa ila hakuna anaye wauliza hizo roho mbaya
ReplyDeletemunataka asinunue nyumba muda wake ukifika muanze kumcheka
Tatizo LA bongo mtu akifanikiwa mara utasikia Freemason mara madawa ya kulevya. Ikiwa mpira wa miguu umetushinda mwecheni dogo apeperushe bendera nchi za nje.!!
ReplyDeleteNdo maaana mademu wanamsumbuaaaa PESA sabuni ya roho,kila DEMU sasa hivi anataka kuchukua nafasi ya wema,akiwemo penny
ReplyDeleteFreemason
ReplyDeleteunamjua freemason au uaandika vitu usivovijua bwege we
Deleteakuna mwana mziki tajiri kama diamond hapa Tz wenye wivu mkachibe shimo mjifukie
ReplyDeletesembe tu huyu, halafu me ndo na "WIVU" na "ROHO" mbaya kwekweli!! sipendi kweil kuona mwingine anaendelea nataka mimi tu!!
ReplyDelete