Tanzania ni Nchi ya 5 Kwa Uchumi Unaokua Kwa Kasi Zaidi Duniani

Wakuu, nilikuwa naangalia kipindi cha "Last Word" cha Lawrence O'Donnell kwenye chanel ya msnbc, na kati ya mambo yaliyoongelewa ni mkutano kati ya USA na viongozi wa Africa. Jambo lililonigusa zaidi na kupelekea niweke uzi huu ni kusikia kwamba Tanzania ni kati ya nchi 10 zenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi duniani. Kwenye orodha ninayoambatisha hapa chini imeorodheshwa kuwa nchi ya 5.
Ebu tujadili hilo kwa mtazamo chanya kuona ni jinsi gani kasi hiyo ya kukua kwa uchumi inawagusa na kuwanufaisha wananchi.
Naomba economists watusaidie kuelewa hili.
Nawasilisha.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera sana rais wetu.. sisi hatukuthamini ila wajuz wa mambo wanaojua kupima uchumi kila leo wanakumwagia tuzo.. na hakika sioni wa kupokea kijiti chako zaid ya lowasa but wengine ndani ya chama chako na hata hao wapinzani kwa kweli hakuna.. sema hela huku mtaani kwa miezi minne hii imekimbia, kidogo umewapa hali ngumu wananchi wako na hisi bunge la katiba linachangia coz kulipana laki tatu kwa mwezi kwa mbunge mmoja kwa cku miez yote hiyo sio kitu cha maskhara!!! Na hapo kuna gharama nyingine za kuendesha bunge hilo, nimestuka zaid kuona umeliongezea cku stini hakyamungu hali yetu cc wabangaizaji mtaani cjui itakuaje.. naomba ka vipi livunjilie mbalin coz output ya huo mjadala wa idadi ya serikali mbona inafahamika.. ni serikali mbili hata ukawa waandamane uchi.. so okoa wananchi wako bunge lako la katiba linatupa njaa.. livunje na sisi tufaidi kupanda kwa uchumi!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad