Hili liko wazi kabisa kuwa TBC1 na TBC FM badala ya kuwa chombo chenye maslahi kwa Taifa zima yaani wenye vyama na wasio na vyama lakini imegeuka kuwa chombo cha matangazo na uenezi wa CCM.
Taarifa zinazohusiana na mafanikio katika mikutano ya vyama vya upinzani ama asasi zenye mtazamo tofauti na CCM hazirushwi na Tv wala redio ya Taifa isipokuwa ya CCM ama vikundi vinavyoisifia CCM.
Makongamano mengi yanayofanyika nchini kuelimisha wananchi kuhusiana na mustakabali wa Taifa letu hayarushwi hata kwa kuchukuliwa vipannde hasa vinavyoikosoa serikali ya CCM.
Nadhani ninyi nyote ni mashahidi.
Je, nani anabisha na kwanini?
Hongera ITV Angalau Mpo Katikati na Mnaonesha vipindi Bila Kuwa Mlango wowote wa Kisiasa..
Kweli hakuna longolongo.sasa si wabadili jina waite ccm brodcasting telivision.
ReplyDeleteNi kweli kabisa ITV mko juu sana kwa kutuelimisha hilo halina ubishi sasa hiv taarifa ya habari inayoangaliwa kwa wingi ni ITV!mko juuuuu!
ReplyDeleteSikumbuki lini mara ya mwisho kuangalia taarifa ya habari ya tbc! Mayb kipindi Tido Muhando alivyokuepo aliibadilisha.
ReplyDeleteMinaking'amuzi ILA taarifa ya habari Yao stizami natizama ya chnel 10,itv, na star tv.wao nawaonaga wazushi tu na ccm Yao.itv mengi Yuko vzuri sio mnaleta habari zakusifia ccm tu nisawa uwe nadini uwazarau wenzio unaona dini yako ya thamani.siwafagilii tbc hatakidogo wababaifusana.
ReplyDeleteHata watangazaji wake wako serious utadhani wako kwenye chumba cha mtihani was hesabu mfano Gabriel Zacharia akitangaza taarifa ya habari mie hua nahic ananifokea so naamua ku-tune Star Tv
ReplyDeleteKama huangalii TBC, umemjuaje Gabriel Zakaria? Na hatakama msipoangalia, mishahara yetu iko pale pale......mpo!
ReplyDelete