NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ambaye hivi karibuni ndoa yake iliripotiwa kuwa katika sintofahamu na kuvunjika, anadaiwa kuhamia katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Oysterbay jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa akionekana akiingia na kutoka kwenye hoteli hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara-Temboni, Dar ikiwa haina mkazi wa kudumu.
Wiki iliyopita, kulienea taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuvunjika kwa ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel Fikirini Habash. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005.
Taarifa zikadai kwamba Gardner naye aliondoka nyumbani hapo na kwamba hivi sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake.
Hata hivyo, gazeti dada ya hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita lilizungumza na Gardner ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, lakini alikanusha vikali uvumi huo akisema si kweli.
Kufuatia madai hayo, mapaparazi wetu walikwenda hadi nyumbani kwa nyota hao ambapo hakukuonekana dalili za kuwepo kwa mtu ndani.
Baadhi ya majirani walioulizwa, walisema mara ya mwisho walimuona Gardner miezi miwili iliyopita akiwa na basi la Bendi ya Machozi lakini hawaelewi kwa sasa wanaishi wapi na wakoje katika ndoa yao!
Juzi, mapaparazi wetu walipiga kambi hotelini hapo ambapo mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo alisema, Jide anaishi hotelini hapo na kwamba kutokana na kuwa mteja wa muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango wa chumba chake anaondoka nayo.
Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Jide (jina tunalo) alithibitisha msanii huyo kuishi hotelini hapo ingawa alikataa kuzungumza lolote kuhusu ndoa hiyo, kwa kile alichodai kuwa haieleweki.“Ni kweli Anaconda (Jide) anaishi pale, wewe nenda tu mapokezi kaulize utaelezwa kama hivi sasa yupo au hayupo,” alisema mtu huyo.
Juhudi za kutafuta ukweli wa sakata la nyota hao zinaendelea huku ikielezwa kuwa, Gardner ndiye anayetakiwa kutoa tamko kwani ndiye anayepatika kirahisi katika simu yake ya mkononi.
Tetesi za Kuvunjika Kwa Ndoa Yake JAY DEE Ahamia Hotelini
14
August 21, 2014
Tags
Ndio maisha ya sasa ya wanawake mastaa kuhamia mahotelini mara wanapotofautiana na waume zao ,au?Mimi tutabanana humuhumu ndani kwangu labda ahame yeye( mume).
ReplyDeletembona hizi movie zinafanana....dida,jide na flora?tatizo nini wadau?
ReplyDeletewana pesa,mie kapuku nitaanzaje kukaa hotelini?
DeleteTatizo ni dharau kwa waume zao, kama unamuheshimu na kumpenda mumeo hata kama 'kapuku' huwezi kumdhalilisha hata kidogo, tena utafanya juu chini watu waijue kwamba mumeo ni 'apeche alolo'.
Deletewe akili hewa inaonesha ni jinsi gani familia yenu mlivyo magolikipa mkisujudia midume kama miungu hebu tuondolee fikira mgando zako mfyuuuu
Deleteakaetuhuko mwakamzima kwanishida nini?kila lakheri hamia kabisa nakwako kimara pangisha.utulie usubiri mume mwema kutoka kwa bwana uombe mungu safari hii usitumie ndumba tena.uwe naimani na mungu uone km hutapata ilawakati huo nawe uwe mkemwema maana nimbishisana unajibishana namumeo mpk kwa tv kisa nipesa basikaaga bilamume ili uwe mbishi forever.hatakama mumeo muhuni anayake siulimpenda mwenyewe ukamkazania mtii tu au ulifikiri ndumba zingemfanya awe zoba siwote zinawakubali nahuwazinaisha nguvu karinyuu tena au omba mungu kila lakheri
ReplyDeletekwani Talaka tatizo?,mbona wanaume wanawapa talaka wanawake zao bila wasiwasi na maisha yanendelea,kukaa kwenye ndoa hata miaka 20 kama mambo hayaendi sawa ni bora kutengana kila mtu kimpango wake,tatizo tunajua kushabikia vitu tusivyo vijua na niwepesi wa kusema mwanamke avumulie tu, kuna tabia zingine hazivumiliki,peaneni nasafi kwa muda,
ReplyDeletehebu chukua kreti la bia kwa mangi kunywa nitalipia umenena kwa lugha. Unajua kuna mijike mingine humu ndani haina akili, ndoa haikuhusu unashabikia hovyo kwasababu maisha ya peke yake, VUMILIA YAKO mengine hayakuhusu.
DeleteMalipo ni hapahapa duniani,kwa Mungu ni hesabu tu.
ReplyDeleteKumbuka G alikuwa na mke na mtoto,akamuacha akakuoa wewe,kwa nini hukujiuliza na kutaka kujua kisa cha kuacha mke na kuja kwako?ulijiona wewe ni dhahabu na kwamba utang'aa wakati wote eeeeh,!sasa leo unahama nyumba yako,kesho utauza,wee subiri tu.
Eeeh,kweli mdau.Wanawake tunapoolewa kwa mwanaume ambae alishawahi kuoa ni bora umkute mwanaume huyo ameachana na mke wake kwa sababu zao zingine kabisa,lakini wewe usiwe ndio sababu ya wao kuachana.
DeleteKimenuka kwelikweli!
ReplyDeleteNitahama chumba lakini sio nyumba,unahama nyumba kumpisha au kumuogopa mume au?
ReplyDeleteKama ungekuwa na watoto wangekuja kukusalimia hoteli kila siku?
SAFI MDAU,NA WANAOFANYA HIVI WANA JEURI YA HELA NA WATOTO WAO WAKO SHULE ZA BWENI,AU UTAKUTA HAWAJAZAA KABISA.TATIZO TUNADANGANYANA SANA WANAWAKE,KAMA NI TALAKA SI ITAKUKUTA HUMOHUMO NDANI KWENU?KWA NINI UHAMIE HOTELINI?
Deleteukiona mwanamke anahamia hotelini ujue anajiamini,mimi nikitibuana na mume wangu kwanini nikae umo ndani?kwani nikimuona tu kichefuchefu.si bora nisepe tusionane ana kwa ana?kuama chumba ni kujichora tu na kama una watoto ndo kabisaaa,hotelini ndo mpango mzima,tatizo 90% ya wanawake wana wategemea wanaume zao hela za kuamia hotelini ni shiiiiiiida watazipata wapi?
Delete