Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa watu wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.
Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake binti huyo alinynyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo cha binti huyo, ukweli tu kwamba mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.
Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu na kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususan cha mtu maarufu.
Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki, wanaharamu na kila aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza. Kwa Twitter, matusi imekuwa ni njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, na ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'
Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria na wanajifahamu. Japo sijui chanzo cha 'ugomvi na aliogombana nao' (na ndio maana sikujihusisha nao kwani haukunihusu), kuna wanafiki wengi tu waliokuwa katika nafasi nzuri ya kuzima moto huo hasa kwa vile baadhi yao walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika.
La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni unafiki: baadhi ya watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa, katika hali ya utani japo wenye uweli, kwamba 'wakati mwafaka kabisa wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.
Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali
Hata pasi uelewa wa taaluma ya saikolojia, tweets za aina hii zinaashiria tatizo, na laiti 'wenye upendo wa dhati' wangeingilia kati muda huo, huenda muda huu Betty asingekuwa marehemu.
Na hizo tweets mbili ambazo ni miongoni mwa za mwisho kabisa za marehemu ni ushuhuda tosha wa jinsi alivyokuwa akisumbuliwa na wanyanyasaji dhidi yake mtandaoni. Ndio pengine kilichomuua ni maradhi ya kawaida ya kibinadamu lakini kila mwenye ubinadamu hatoshindwa kuhusisha unyanyasaji huu na hali mbaya ya afya aliyokuwa nayo hadi anafariki.
Kuna watakaolaumu kuwa ninatumia kifo cha binti huyo kwa 'maslahi binafsi.' Hapana, sina maslahi yoyote binafsi hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nikifahamiana na marehemu. Hakuna anani-follow na mie sikuwa nam-follow. Labda maslahi pekee niliyonayo ni upinzani wangu mkali dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni. Vyovyote ilivyo, marehemu alikuwa bullied kabla hajafariki na atakayetaka kukataa ukweli huo na akatae lakini utabaki kuwa ukweli usioweza kugeuka uongo. Na kwa hakika, kila aliyeshiriki kumnyanyasa binti huyo atakuwa anasutwa na nafsi yake, hata kama atatafuta hifadhi kwenye 'huu sio wakati wa kulaumiana' au 'we failed you Betty.'
Mara nyingi nimekuwa nikiwalaumu watu wanaodai 'Instagram imekuwa mbaya' au Twitter imeharibika siku hizi' ambapo mara zote nimewakumbusha wahusika kuwa katika hii mitandao ya kijamii, ni muhimu kuwa makini katika nani wa kum-follow. Maana yangu ni kwamba ukim-follow mtu mwenye matusi, utashuhudia matusi katika anachoandika. Ukim-follow mtu wa busara, utashuhudia busara.
Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa tu la watu wenye busara na elimu zao lakini wepesi wa kuvutiwa na vitu vya 'kipuuzi' - umbeya, matusi, majungu, na upuuzi mwingine, na hawasiti kushea na wanaowa-follow. Ni hivi, mtu akitweet tusi, kisha ukali-retweet, utambue kuwa unalikuza (amplify) tusi hilo. Na kimsingi, kwa kiasi kikubwa, tuna-RT vitu tunavyoviunga mkono. Uki-RT tusi maana yake unaliunga mkono. Na ni wazi mwenye kujiheshimu, na kuheshimu 'watu wa maana' wanaom-follow hawezi ku-RT upuuzi.
Tatizo kubwa sasa ni kwamba waweza kuamua kuwa-follow watu unaodhani wana busara au akili za kutosha lakini ukaishia kusoma vitu vya ajabu ajabu kwenye timeline yako kutokana na haya 'mahaba' ya ku-RT vitu vya kipuuzi.
Binafsi, nadhani chanzo kikubwa cha mitandao ya kijamii kuwa 'sehemu za kukera, kuogopesha, kunyanyasana, nk' ni ile hali ya baadhi ya wenzetu kutokuwa na vitu muhimu vya kufanya katika maisha yao. Ni wazi kwamba ukiwa busy na maisha yako hutokuwa na muda wa kubughudhi wenzako.
Kingine kinachopelekea social media kuwa 'dunia uwanja wa fujo' ni ugonjwa mkubwa unawasumbua baadhi ya wenzetu: kusaka sifa wasizostahili. Wanasema,. ashakum si matusi, 'lugha ya mpumbavu ni matusi,' na ndo maana baadhi ya wenzetu wasio na cha maana cha kuongea katika hadhara hukimbili matusi, unyanyasaji, maneno macha
Nitamke bayana kuwa siandiki makala hii nikitegemea kuungwa mkono na wahusika wa unyanyasaji mtandaoni. Na kwa hakika kuna uwezekano mkubwa wa makala hii kuzua 'kampeni ya chuki' dhidi yangu kutokana na makala hii. Tatizo kubwa la wenzetu hawa ni kutotaka kuambiwa kuwa 'Hapana, hili ni kosa. Na kosa ni kosa, haliwezi kuwa sahihi.' Lakini pamoja na uwezekano wa 'kuwashiwa moto' kutokana na makala hii, wito wangu kwa kila mwenye busara na akili ni kuliangalia tukio hili la kusikitisha kama 'wake up call.' Tujifunze, tujisahihishe. Tuache kusherehesha vitu vya kipuuzi mtandaoni.
Ifike mahala, ukishindwa kumkemea mtu mwenye tabia mbaya mtandaoni basi chukua option rahisi ya kum-unfollow au ikibidi kum-block. Na ifike mahala kuwafahamisha watu wanaoendekeza utoto, majungu, umbeya, unyanyasaji na upuuzi mwingine kuwa kama hawana kitu cha maana cha kufany katika maisha yao basi isiwe sababu ya kuwasumbua wenzao wenye majukumu katika maisha yao.
Tukemee maovu badala ya kutarajia yataondoka yenyewe tu. Tuomboleze kifo cha Betty kwa kusema 'NO' kwa cyberbullies (wanyanyasaji wa mtandaoni). Tufike sehemu tuache kuwasujudia wahuni wanaodhani matusi ni sehemu ya wimbo wa taifa. Tuwakwepe waendekeza majungu, wanyanyasaji, wataka sifa za kipuuzi, na watu wasiofaa katik maisha yetu.
Wakati 'tunatafuta haki kwa marehemu Betty kutokana na unyama aliofanyiwa,' suala ambalo ni la kisheria, kilicho ndani ya uwezo wetu ni kukemea unyanyasaji mtandaoni (cyber bullying). Wakati hadi muda huu hatuwajui waliomfanyia marehemu unyama huo, takriban sote twawajua vema wanyanyasaji wa mtandaoni. Tuanze na hawa, kwani leo wamefanya kwa kwa marehemu Betty kesho itakuwa kwako.
Mwisho kabisa, ni muhimu kwetu sote kutambua kuwa tulitoka kwa udongo na tutarudi kwa udongo. Kifo ni hatma ya kila mmoja wetu.Betty ametutoka lakini nasi twaelekea huko. Visa, chuki, kunyanyasana, na vitu vingine visivyopendeza japo ni kama sehemu ya maisha yetu havipaswi kupewa nafasi katika maisha yetu haya ambayo hakuna mmoja wetu mwenye japo 'lue' ya lini yatafikia kikomo. TUPENDANE na TUHESHIMIANE.
Kwako marehemu Betty, hakuna tunaloweza kusema au kufanya sasa kurejesha uhai wako. Na hakuna neno sahihi la kuonyesha jinsi gani kifo chako kimewagusa wengi. Kubwa tunaloweza kufanya ni kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akupatie pumziko la milele na mwanga wa milele akuangazie upumzike kwa amani. Amina.
Evarist Chahali
R.I.P Betty haki itatendeka, hata kama hao watu watajificha vipi but watalipwa zaidi ya walivyokutenda
ReplyDeleteMungu ilaze roho yake mahala pema peponi,simfahamu lakini namwomba mwenyezi mungu aliyejuu haki itendeke haraka iwezekanavyo na tushuhudie, kwan who are they to take someone's life like that if they are not the creator dont let them go dear God.
ReplyDeleteSasa na nyie waandishi ..KWANINI HAMSEMI AMEKUFAJE? YANI MATUSI UNYANYASAJI MITANDAONI NDIYO UMEMFANYA AKAFA KIVIPI ?????????.......Andikeni habari mkiwa unalengo la kusomwa na kueleweka..........BONGO BLOGGERS ....Igeni Flora Lyimo Blogs na Michuzi ......na baadhi ya zinine kama tatu hivi ndizo huandika kabari za ukweli na zinazoeleweka''''' mfyuuuuuuuuuu'''
ReplyDeleteze la udaku si bogasi tu hata elimu yake ndogo sana copy paste kibao hana uwezo wa kuandika makala pia hajua kusema katoa wapi hapi just plain ziro ziro kichwani
Deletehow did she die ????????????????
ReplyDeleteSaa chache kabla ya kifo chake Betty alitweet kua "PINDA HAWEZI KUWA RAIS". Baada ya kutweet hakuonekana tena hadi alipookotwa mtaroni kesho yake asubuhi akiwa amefanyia vitendo vya kikatili na akiwa amepoteza fahamu.
ReplyDeleteLakini kabla hata ya kutweet hivyo, Betty alikua anaandamwa sana mtandaoni huko Twitter. Kuna watu walianzisha team ya kumtukana, kumjibu hovyo na kumprovoke kwa kila alilofanya.
Betty akiwa katika maumivu makali ya hisia akapost hivi "Thank you all for the names i was called, luck y'all have such a perfect life.! No hard feelings.. Im alive still.! Endeleeni kuongea"
Kwa tafsiri isiyo rasmi Betty alisema "Asanteni kwa majina yote mliyoniita. Mmebarikiwa kuwa na maisha mazuri.! Hamuumizwi na hisia kama mimi. Ila bado ninaishi, endeleeni kuongea"
Kwa bahati mbaya hakuna aliyejali, hadi juzi asubuhi (jumatano) Betty alipookotwa kwenye mtaro akiwa amefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na akiwa amepoteza fahamu.i na kupelekwa hospitali. Jana (alhamisi) aliweza kufungua macho, lakini hakuweza kuongea lolote hadi saa 3 usiku wa kuamkia leo, mauti ilipomkuta.
Kifo cha Betty ni miongoni mwa vifo vya kikatili sana kuwahi kutokea nchini
Mimi namshangaaa huyu mwandishi wa hii nakala the way anavyoonyesha undumilakuwili katika hilo suala. Anaelewa kabisa ukweli wa mauti yaliyomkuta marehemu Betty lakini kwa makusudi kabisa anajaribu kupindisha ukweli wa mambo ili ionekane Cyber bullying kama ndio chanzo cha mauti yake Betty. Huyo mwandishi amedhihirisha jinsi alivyokuwa kibaraka wa hilo tabaka la watawala na jinsi anavyotumika kulilinda kwa nguvu zote juu ya maovu makubwa wanayoyafanya. Kwani ni nani ambaye haelewi tatizo la cyber bullying hapa Duniani? Ni kweli kumekuwa na matatizo ya Cyber bullying katika hizo Social Networks lakini mazingira ya kifo cha Betty haya suggest kwa namna yoyote ile kama ni kweli ilitokana na hiyo pressure ya kwenye social networks. Ikumbukwe ya kuwa kabla ya kuanza kushambuliwa kwa kunyanyaswa na hatimaye mauti kumkuta ni kwamba marehemu Betty ali tweet maoni yake ya kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mazengo Pinda hawezi kuwa Rais wa Taifa la Tanzania. Na pia ikumbukwe ya kuwa huyo huyo Waziri Mkuu Mazengo Pinda aliwahi kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya wapenda demokrasia Tanzania nzima na kuyafananisha maoni yao kama ni fujo. Na pia vyombo vya Habari vilimnukuu akisema kuwa hawa watu "WATAPIGWA TU". Sasa tunajuaje kama ni kweli huyo marehemu Betty ni victim wa hiyo kauli ya Waziri Mkuu Mazengo Pinda kisa ametoa maoni yake ambayo kimsingi yalikuwa ysnamhusu moja kwa moja huyo Waziri Mkuu Mazengo Pinda. Kwa kweli ni aibu na ni so devastating. Tunajua kuwa vyombo vya sheria havitachukua hatua zozote zile uchunguzi wa kina katika suala hilo kulingana na dhana ile ile ya kulindana. Mwandishi wa hiyo nakala anachofanya ni kutuletea dhihaka watanzania kana kwamba vichwa vyetu vimelala na bila ya aibu anatumia nguvu ya kalamu yake kupindisha ukweli wa mambo.
ReplyDeleteR.I.P. Betty Ndejembi!!
Halafu huyo mwandishi wa hiyo nakala jinsi alivyokuwa hypocritical anasema bila ya aibu eti tuomboleze msiba wa Betty Ndejembi kwa kusema No To Cyber Bullying. Anasahau kama hayo mauti yaliyomkuta masikini Betty mtoto asiyekuwa na hatia ni matokeo ya wale viongozi walafi wasiotaka mabadiliko wala uhuru wa kujieleza maoni yao wananchi. Hao ni viongozi aina ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Kwa nini isiwe "NO TO AUTOCRATIC LEADERS". Sasa huyu ni aina ya kiongozi ambaye watu wanaanza kupoteza maisha yao kwa kisa cha kutoa maoni yao dhidi yake katika hiki kipindi ambacho hajaingia pale magogoni/Ikulu. Unajaribu kufikiria ni watu wangapi watakaopoteza maisha yao kwa kusema ukweli wa mambo pale atakapobahatika kushika Nchi. Kwa kweli ni aibu na mikosi kwa kiongozi wa position yake kama Waziri Mkuu wa Nchi pamoja na watu wake. Ni aibuuuuu. Huyo mwandishi wa hiyo nakala pliiizzz hebu tuondoleee huo umburulazzz wako kwa kutumika kama kibaraka ili kuyalinda maovu ya wakubwa. Tunajua una njaaa lakini ni lazima uwe na hofu na roho za watu innocent kwani hiyo njaaa yako kuna siku itaisha kwa nguvu ya umma.
ReplyDeleteR.I.P. Betty Ndejembi!
Nahisi kama kuna kitu unakijua juu ya kifo cha Betty,na pengine Betty aliwahi kuongea na wewe siku za nyuma kabla ya kufanyiwa huu ukatili lakini unaogopa kusema,fanya unavyoweza liwe wazi,si lazima kwenye mitandao kama hivi la hasha,please,I know you can do.DO IT.
DeleteInasikitisha kama kuna ukweli,lakini hakuna kitu kitafanyika juu ya hili "hata kama kuna ukweli".
ReplyDeletetumuombee,amekwenda,ni njia ya wote.
R.I.P. Betty.
Msenge aliefanya huyu mtoto akafa msenge jazz band........
ReplyDeleteMwingine anayenyanyasa wenzio kwenye mitandao wa instragram, n huyu so called usipojipanga ntakupanga, kila siku Diva Diva, c umwache diva wawa2 utamuuua mwenzio
ReplyDeleteHuyo mwandishi wa hiyo nakala kwa jinsi alivyokuwa mburulazzz na anavyotuonyesha jinsi asivyojiamini katika kazi yake utaona ameanza hiyo nakala kwa kujitetea kwa kusema eti anajua hiyo nakala itawaudhi wale watu wanaongia kwenye Social Networks kuwanyanyasa watu na pia anaendelea kwa kusema eti hiyo haiondoi ukweli wa kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Kwa kweli hapo amejidhihaki na pia kuidhihaki taaluma nzima ya uandishi wa habari. Hiyo inaonyesha jinsi gani asivyojiamini na pili jinsi alivyotumwa kuiandika hiyo nakala kwa lengo lile lile la kuwalinda wakubwa. Halafu kwa kuonyesha jinsi alivyokuwa kibaraka wa watawala anaendelea kupindisha ukweli wa mambo kwa kutueleza jinsi marehemu alivyonyanyaswa kwenye Twitter siku chache kabla ya kifo chake huku kwa makusudi kabisa akikwepa ukweli wa chanzo cha minyanyaso hiyo ambayo kimsingi ilisababishwa na maoni na mtizamo wake binafsi dhidi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ya kugombea Urais wa Nchi ya Tanzania. Unaona huyu mwandishi wa hii nakala kwa jinsi alivyokuwa mburulazzz anajifanya eti hadhamiriii kumlaumu mtu yoyote bali ni kutoa rambirambi zake kwa marehemu na pia kulizingumzia kwa undani tatizo la Cyber Bullying kwenye Social Networks. Unaona sasa anajitahidi kwa nguvu zote kuwaondoa wasomaji wa hiyo nakala katika kujikita katika suala la msingi lililopelekea marehemu Betty kupoteza maisha ambalo kimsingi ni maoni yake aliyoyatoa dhidi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na ambayo kimsingi hayakuwa na ubaya wowote. Pia mwandishi wa hii nakala anajikita zaidi katika kupoteza lengo kwa kusimulia zile story za alinacha na pia kudai kuwa marehemu alidhalilishwa na kutukanwa kwa kuitwa majina mbalimbali na anatueleza hajui chanzo cha ugomvi kwa wale aliogombana nao. Hii kimsingi ni dhihaka ya hali ya juu kwa watanzania. Huyu mtoto masikini asiyekuwa na makosa alikuwa anatukanwa na watu wa huyo Waziri Mkuu Mizengo Pinda kujifanya kwamba haujui chanzo cha ugomvi huo kimsingi ni unafiki wa hali ya juuu. Huyo mwandishi wa hiyo nakala anaendelea kudhihirisha unafiki wake pale anaposema hatumii hicho kifo kilichomkuta marehemu Betty kwa maslahi yake binafsi. Huyo mwandishi wa hiyo nakala ni kibaraka mkubwa na pia ametumwa ku cover maovu ya wakubwa. Huyu mwandishi ni kilaza amejitetea mno na very unnecessary unaona maneno kama eti hategemei kuungwa mkono na wahusika wa unyanyasaji kwenye hizo Social Networks kwa kweli ni so pathetic. Huyu mwandishi amekwepa kufanya discussion ya ile core issue iliyopelekea kifo cha marehemu. Jamani watanzania wenzangu ni lazima tuwe makini na aina hii ya waandishi uchwara na vibaraka wanaotumika kufunika maovu ya watawala. Unajaribu ku imagine jinsi watu wanavyokosa ile honesty na transparency katika jambo kama hili je inakuwaje inapokuja kuandika mambo yenye maslahi makubwa kwa Taifa la Tanzania na hasa yale yanayowahusu walalahoi. Hawa ndio aina ya waandishi wetu. So ridiculous!
ReplyDeleteHao watu wote walikuwa wanamshambulia na kumnyanyasa marehemu Betty ni watu walio nyuma ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na huyo Mizengo Pinda analielewa hilo. Na huyo mwandishi wa hiyo nakala kibaraka pia analielewa hilo. Hii ni karne nyingine. UHURU WA MAWAZO NA MAONI YA WATU NI LAZIMA UZINGATIWE!!
R.I.P.Betty Ndejembi!!!!!!!
Hawa Wazee viongozi aina ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda hawataki kuamini kama uzee wao umefikia kikomo na kwamba huu ni wakati wa vijana kuendesha nchi. Vijana ndio Taifa la kesho. Vijana ndio rasilimali na nguvu ya Taifa la Tanzania. Wameng'ang'ania madaraka hawataki kutoka. Hawataki kuwapisha Vijana. Hawataki mawazo mapya sasa haya ndio matokeo ya aina hii ya viongozi walafi wa madaraka. Wanaishia kuwaua watoto wa watu waiokuwa na hatia. Kisa kikiwa ni mtizamo tofauti na wao. Kwa kweli Mungu utusamehe sana.
ReplyDeleteR.I.P. Betty Ndejembi!!
"HATIMAYE ZILE MBIO ZA URAIS TANZANIA ZAANZA KULETA MAAFA." Masikini kale katoto ka watu KameKolimbwa. Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi. Amen!!
ReplyDeletehuyo Mizengo pinda. Watu tukitoa kula zetu , tuandike tumeumia hakuna madiliko yoyote yatakayotokea, unafuu au afadhali itakuvyote ziiiiiiii, uwo uwaziri tu michosho ndio utakuwa Uraisi hmmmm, Kwa Loasa hapo kweli hata mwanga unaonyesha jamani, huyo pinda ni michosho tu,hamna mwanga hapo
ReplyDeleteHuyo Waziri Mkuu Mizengo Pinda atafaaa vipi kuwa kiongozi wa Nchi kama Tanzania????? Huyu mtu hatufai. Huyu ni kiongozi ambaye amepata msukumo wa kugombea hiyo nafasi ya juu ya uongozi katika Nchi eti kwa sababu tu ameshauriwa na Mapadri, Maaskofu na Mke wake. Huyu ni kiongozi ambaye hakusukmwa na matatizo na changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ya Tanzania kama kuinua hali za wananchi kutoka katika lindi la umaskini, kuendeleza miuondo mbinu na hata kutueleza ni strategies gani anazo ambazo atazitumia kuondoa tatizo la ajira linaloikabili jamii na hasa vijana ambao kimahesabu ndio walio wengi na ndio waathirika. Kimsingi huyu kiongozi hana agenda yoyote ya maana ya kumfanya awe kiongozi bora wa kuliongoza Taifa kama la Tanzania. Sasa angalia hiyo tamaa inavyompeleka pabaya. Watoto na vijana ambao ndio msingi na rasilimali kuu ya Taifa wameanza kupoteza maisha kikatili kwa sababu tu ya kuwa na mtizamo tofauti na yeye. Huyu kiongozi HATUFAI.
DeleteAtaongoza nini Huyo pinda si atapindisha nchi tu, kwanza, asije leta Udini wake tu, ikiwa ushauli apate mpaka kwa masikofu na mapadri hapo kweli kinaeleweka, Udini na siasa wapi? na wapi, viongozi kama hawa ni wa kuwakimbia kama ukoma, hawafai katika jamii kwanza hawajengi Taifa bali wanalibu Taifa, uwazri wenyewe tu anajikongongoja, Jamani Tanzania limeshakuwa Taifa kubwa katika Africa, na sio Taifa changa, laitaji kiongozi imara ili liweze songa mbele, kutoka kizazi mpka kizazi, sio kuharibu, huko ikuru mbona wana kukimbilia sana kunani kwani, nyerere si alisha wambia Ikuru sio sehemu ya kukimbilia. hawaigi mfano tu, au ndio mikubwa jinga
Deletejamani wapendwa hii habari ni kwangu mimi sijaelewa vizuri huyu dada aliyeuwawa nina nani kaika jamii i mean ni mcheza movie au ni miss au mbunge nijuzeni wapendwa niko gizani
ReplyDeleteUko gizani kwa sababu ni mpumbavu. Kwako wewe ni lazima awe mjinga au Kicheche kutoka Bongo Movie au Bongo Flava huo ni upumbavu. Huna akili yoyote ya kufikiria kuwa raia wote wa Nchi husika wana uzito sawa ukiachilia mbali nafasi zao katika jamii. Huyu ni msichana mdogo mpendwa ambaye ni raia wa Nchi tukufu ya Tanzania ambaye ameuwawa kikatili na watu wanaopinga mawazo na maoni huru dhidi yao. Huyu msichana ambaye kulingana na umri wake bado alikuwa na nafasi ya kutosha ya kuleta mabadiliko ya kimsingi katika Nchi ya Tanzania kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hiyo nchi. Na hasa ukizingatia ni kijana kama vijana wengine. Wewe anonymous hapo juu achana na dhana hiyo potofu kwamba mtu ni lazima awe Mbunge au awe ametoka Bongo Movie. Dhana potofu kama hiyo haiwezi kukusaidia lolote katika harakati zako za maisha na hasa kama ni kijana. Acha upunguani.
DeleteSasa kunyanyaswa kijinsia wanamaanisha hao wahuni walimbaka? Mbona mnapindisha kiswahili namna hii. Hao wahuni lazima wakamatwe wateswe adi wamtaje aliewatuma. Mdau hapo juu Betty alikuwa ni mwanamitindo.
ReplyDeleteR.I.P Betty Ndejembi!!
Ndio maana yake mdau juu. Yaani pamoja na mambo mengine ya kikatili waliyomfanyia moja wapo ikiwemo kumbaka. Huo ndio uhalisia wa mambo uliopelekea mauti yake. Huyo ndio yule Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na watu wake wanavyoutafuta Urais wa Nchi kwa nguvu. Kwa kweli mpaka uchaguzi mkuu utakapofika kazi ipo ni jambo la kusikitisha sana.
DeleteMungu wangu ..jamani mbona mnaogopesha watu sasa..........? yani haiwezekani Waziri Mkuu PINDA ..Got anything to do with this............kwa kweli huyu Msichana inafaa afuatiliwe vizuri ...haiwezekani mtu agombane na watu alafu muanze kufuatilia comments zake au mambo ambayo alikuwa kaandika kala ya kifo chake...yani haiwezekani kamwe kihivyo ...cha msingi ..wewe muandishi wa habari hii...UNATAKIWA KUJUA JINSI YA KUANDIKA HABARI KAMA HIZI,,,TUAMBIE KUHUSU MAREHEMU...HOW SHE DIE...WHERE ,AND JE KUNA MTU YOYOTE WA KARIBU WA MAREHE? HANA NDUGU KABISA ? YANI KUSEMA UKWELI ..I THINK SASA NI VEMA BLOGS ZOTE ZA BONGO KUTOKURUHUSIWA KUTANGAZA HABARI ZA WATU BILA KUWA NA HABARI ZA KUWAHUSU KAMILI.....SO SAD....BADO HII SAD HABARI INAZIDI KUHUZUNISHA .....
ReplyDeleteKwa hiyo amekufa kwa ajili ya KUBAKWA ???? Yesu na Maria............Hivi mbona naona kama hii habari ni ndito kuliko maji ? walimbakia wapi na aliokotwa mto upi ? please guys tupeni habari za kueleweka ...Yani msichukulie hichi kama kitu cha msaha...KUMBUKENI KUNA FLORA LYIMO ALIDAE KWAMBA MBUNGE WA ARUSHA GODBLESS LEMA KAMBAKA....Sasa unataka kuniambia Flora Lyimo akija bongo sasa hivi itakuwaje ? uwiii...so sad.............NGACHOKA!!!
ReplyDeleteKUMUHUSISHA WAZIRI PINDA NA MAMBO YENU YA KISENGE MATANDAONI SIO HESHIMA, HAKUNA USHAHID WWT KUWA MHESHIMIWA KAHUSIKA, WALA HAKUNA COMENT ALIYOITOA BAADA YA KUMZIHAKI HUMU. ULIMBUKENI WENU WA KUTUMIA MTANDAO KWA PUPA NDO UNAWAPONZA, KUWEN MAKINI NA KAULI ZENU
DeleteNA WASIWASI KUWA WENGI MNATUMIA HUU MTANDAO KISIASA ZAIDI NAWASHAURI TUMIEN VIZURI
DeleteBetty ndio nani eti..labda me ndio mgeni hapa TZ!
ReplyDeleteEbu mmoja anaemjua huyu bety atueleze kwa kina .n nani?? Alikua anafanya nn? Anaishi wapi na tukio la kubakwa na kuokotwa wapi na hospitali ipi alipofia.. wabongo wengi mnaakili fupi sana.. mm sio mfuatiliaji wa siasa ila huwezi nicomvice eti pinda anahusika na mauaji ya huyo dada haiwezekani, mpinzani mmoja tu katumia trick ya kuchafua serikari watu bila kutumia akili zao wameanza kucomet kichwakichwa.. haterz, tunasumbuliwa na hicho kitu chuki iliyopindukia na akili fupi.. em fikirieni kwa kina jaman kweli viongoz hawa wameifanya tanzania iwe maskin na hali ngumu ila hii kumuua huyu bint????? Achen hizo wabongo!!
ReplyDeleteNgachoka........!!!
ReplyDeletemi yangu macho
ReplyDeletemmmh!!!!!
ReplyDeleteehe! mbona stori ya bety imeishia hivyo yaani nafikiri waandishi wamepewa warning fulani cos wapo kimya kuliko kawaida , binti kapotea hivihiv ni blog moja tu imetoa na imeshatupilia mbali tofauti na wakina lech ,unaona hata mazishi huyu hakuna kitu ,au ndo shiiiiiiii ucitheme, tupeni habari jamani betty ndo kapote kulikoni???????
ReplyDelete