Video ya Bomu la Soweto Kuwekwa Hadharani, CHADEMA Kuitisha Mkutano wa Waandishi

Kuna habari japo imewekwa kama tetesi, ina ukweli kwamba CHADEMA wanatarajia kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia sakata la bomu la soweto ambalo mpaka hivi leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali. Inasemekana Mbunge wa Arusha mjini atakuwepo kwenye press hiyo na waandishi wa habari, ambao watapewa video hiyo kama ushahidi ili umma wa watanzania wauone mkanda ambao utatoa taswira chanya kwa wananchi kujua ukweli kuhusu tukio lenyewe.

Habari ambazo zimepatikana ni kwamba CHADEMA wataitisha mkutano na waandishi wa habari kabla ya kurusha video ya bomu la soweto, ambalo lilionyesha wazi jinsi polisi walivyohusika kutekeleza ulipuaji wa bomu.

Mkutano na waandishi wa habari unatarajiwa kuwa siku ya jumapili muda na mahali itatangazwa. 

Tutaendelea ku update kadiri tutakavyokuwa tunapokea taarifa.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wanataka kiki ili wapate kura mwakani.....

    ReplyDelete
  2. Safi Chadema wekeni mambo wasiwasi Police wawe Magaidi kisha wamakamata wasio na hatia kazi yao kuwapa watu kesi za kutunga

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni safi kwani serikali na jeshi lake zinaendeshwa kisiasa, wanakurupuka kukamata watu kisha wanaleta mbwembwe kibao kumbe wanabahatisha.

    ReplyDelete
  4. Jamani nipo ucngizini au wazimu unanianza cjijui??? Bom la soweto?? Lile la south Africa tulilolisoma mpaka kwenye histry au?? Maana kama ni lile na chadema wapi na wapi.. em nisaidieni ufafanuzi jamani kabla cjahic kuchanganyikiwa!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad