Wananchi Wawataka Wanasheria Kuweka Pingamizi Mahakamani ili Bunge Maalum la Katiba Lisitishwe

Wengi wa wananchi wamekuwa wakilalamika sana kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba kuendelea ili hali ukweli ni kuwa kundi la wanaotetea maslahi halisi ya Wananchi (UKAWA) hawapo na pia mwenendo wa kuwatisha wanaotoa elimu na maudhui ya Rasimu ya 2 ya Katiba, kupitia vyombo vya Habari na midahalo, ufahamu ambao ni haki ya kila raia. 

Mitaani, watu wengi wanakasirika pia kuwa Taasisi ya kutetea haki za Binadamu (TLHRC) na Jukwaa la Katiba (JUKATA) kuendelea kutokuchukua hatua za kusheria, ambavyo wanasema ni ishara mbaya na kuwa wanaachia watawala waendelee kufanya wapendavyo kuunda katiba yao kwa kupitia wingi wao na kwa kumtumia Spika ambaye ameshindwa kuwa na dira ya kitaifa. 

Wengi wanatoa maneno ya hasira wakisema kuwa ..."kama Legal and Human Rights Centre (LHRC) mnao uchungu halisia kama tujuavyo, na jinsi walivyoonyesha wajumbe wenyewe wa Tume ya Warioba, tunaomba pamoja na timu ya JUKATA mpeleke 'zuio' mahakamani kuhakikisha kama yafaa Mahakama ilazimishe yafuatayo ili kufanya Bunge la Katiba lizingatie maslahi mapana ya utaifa na sio vikundi: 

Kuamuru Bunge la Katiba Kusitishwa kwa muda ili kuruhusu Wajumbe wote wa Katiba kama walivyoaninishwa ktk sheria kuwepo ndani ya Bunge hilo ili kulinda usawa na haki ya kila mwakilishi.
Kuzuia utekelezaji wa sheria iliyoaifuta tume ya Kutunga Katiba ili iendelee kuelimisha Bunge maana na maudhui ya Rasimu ya pili ili taifa lipate ufahamu unaostahili.
Kuamuru Serikali kuufungua Mtandao wa Tume ya Katiba uliofungwa ili kuwapa wananachi wote uhuru na uwezo wa kupata ufahamu wa mengi yaliyozuiwa wasiyajiue baada ya tovuti hiyo kufungwa.
Kutoa kinga kwa Vyombo vya Habari vinavyolenga kuendesha mijadala ya Wazi katika kuelimisha wananchi kuhusu maudhui ya ufahamu wa Rasimu ya 2 ya Katiba ili waweze kujiandaa kwa ufahamu ufaao kuelekea upigaji wa Kura kama hatua hiyo itafikiwa.
Kutoa tafsiri Kamili ya misingi ya Rasimu kulingana na sheria ya Katiba, na kuhakikisha misingi yake mikuu ya Rasimu ya 2 (ambayo yanatokana na maoni ya Umma) haiguswi au kumomonyolewa au kuvurugwa kwa hila na makundi ya wachache wanaoongozwa na Spika.
Kutoa kinga kwa waliokuwa wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Katiba waendelee kuelimisha wananchi ktk makongamano ya wazi na kuwaongezea ufahamu zaidi maana Rasimu hiyo ndio msingi wa Katiba yao waliyoiomba kwa miaka zaidi ya 30."


Kama TLHRC na JUKATA wanaipata hii, watoe 'what's next' ili wananchi wajue hatma ya haki na maoni yao, ili isiwe too late, na kuwa endapo itaachiwa Katiba itakayoundwa na wachache ikamilike, itakuwa ndio msingi na chanzo cha matatizo makubwa zaidi kitaifa ambayo yangeweza kuwekwa sawa na mahakama mapema kwa sasa! 

Nawasilisha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad