Nimechunguza sana na kuona kwamba wengi sana ya wanaopinga suala la Tanzania kuwa na uraia pacha hawana sababu za msingi za kuupinga. Wengi wao wanapinga kwa ajili tu kuwaonea husuda Watanzania wenzetu waliopata nafasi za kutafuta maisha nje kwa kuwa wao hawana uwezo wa kupata nafasi hizo. Wakiwa na hili akilini, wanatumia visingizio vya kila aina kupinga uraia pacha. Sababu kubwa tatu zinazotolewa dhidi ya uraia pacha ni zifuatazo;
Uraia pacha utaendeleza ufisadi
Uraia pacha utafanya watu wa nje matajiri wanunue ardhi yetu yote
Uraia pacha ni kukosa uzalendo
Uraia pacha na ufisadi
Hivi hili ni la kweli? Je, tunataka kusema wale Watanzania wenzetu walioko diaspora wote ni mafisadi na hiyo ndio sababu ya wao kutaka uraia pacha? Na kweli wao ni mafisadi zaidi ya hawa mafisadi tulio nao humu nchini? Na hawa mafisadi tuliojaza nchini ni raia pacha wa nchi gani? Na ni ufisadi gani ambao mtu akiwa raia pacha ataufanya - kuondoka na shilingi ya Tanzania kupeleka nje? Kutorosha nyara za serikali? Au kuleta fedha za kigeni nchini? Hata kama ni kutorosha nyara na fedha, sheria na kudhibidi hayo mambo, kama money laundering laws, zitakuwa wapi?
Uraia pacha utafanya matajiri wa nje wanunue ardhi yetu yote
Kwani nani aliyesema tukiruhusu uraia pacha ina maana kila mtu aliyeko nje anaruhusiwa kuwa raia wa Tanzania na kuwa raia pacha akiomba uraia wetu? Hii inaonekana kuwa watu hawajui kwamba walengwa wa kwanza wa uraia pacha ni Watanzania ambao wako nje, ambao wengi wao wanaogopa kuchukua uraia wa huko nje wakihofia kupoteza uraia wa Tanzania, kulingana na sheria ya sasa ya uraia. Na walengwa wa pili ni raia wa nje ambao labda wameoa au kuolewa na Watanzania, na wangependa kutambulika kama raia wa Tanzania pia. Na mwisho ni raia wa nje waliokaa sana nchini na kupata ukazi wa kudumu akini bado wana uraia wa kwao. Sasa hili la matajiri kuchukua ardhi yetu linatoka wapi? Na hata kama ukioa au kuoelewa, kuna sheria ambazo hazikuruhusu kuwa raia wa Tanzania mara tu ukioa bali hadi miaka kadhaa ipite ukiwa mkazi wa hapa nchini. Sasa tatizo liko wapi?
Uraia pacha ni kukosa uzalendo
Jamani, hebu tachane na hizi kauli za kipropaganda. Kwani uzalendo maana yake nini au unaonyeshwa kwa vitendo gani kiasi kwamba mwenye uraia pacha aone kuwa na uzalendo pungufu ya yule asiye na uraia pacha? Jambo la kukumbuka hapa ni kwamba wanaotaka uraia pacha wana hiyo ari kwa ajili ya uzalendo walio nao na Tanzania. Japo wameishi nje muda mrefu bado wanaona shida kukata mizizi na nchi yao Tanzania. Angalia kwamba nchi kama Norway na Israel zina raia wengi nje ya nchi kuliko wale walio ndani ya nchi; na hawa walioko nje uzalendo wao haujapungua hata kidogo kwa kuwa tu wamekuwa raia wa huko wanakoishi. Juzi hapa nimesikia Mkurdishi wa Iraq, yeye na mwanae, ambao kwa sasa ni raia wa Sweden, wamerudi Iraq kwenda kupigana dhidi ya ISIS. Sasa anayesema uraia pacha ni kukosa uzalendo, ni kwa kigezo kipi?
Acha kubwabwaja. Tupe faida za uraia pacha na jinsi Nchi ya Tanzania itakavyonufaika. Kwa sasa ukweli wa mambo ni kuwa Tanzania Diaspora haina nguvu ya kutosha na iliyosheheni kukidhi mahitaji ya kupewa huo Uraia pacha. Kwa ufupi wengi wao sio ma expert sana wa kusema Nchi iko so desperate inawahitaji ama kuna siku itawahitaji. Pia tunaomba utueleze kwa huo uraia pacha utawadhibiti vipi Wahindi ikiwa leo hii tu imeshindikana?
ReplyDeleteNa pia kuna hatari ya Watanzania hasa walio nje ya Nchi kutumia hiyo fursa vibaya kwa kuwapachika watu ambao kimsingi sio wazawa kufanya uhujumu uchumi wa Nchi. Kwa mawazo yangu Taifa la Tanzania bado ni changa mno kujitumbukiza kwa uraia pacha. Ni Taifa ambalo bado linayumbayumba katika mihimili mingi ikiwemo ya kisheria, Ufisadi uliokithiri na hata katika suala linalohusu uzalendo wa Nchi ni watanzania wachache sana wenye uzalendo wa kweli na nchi yao. Kwa hiyo ni lazima tuwe makini katika kutoa mianya ambayo baadae tutakuja kujuta. Kwani majuto ni mjukuuu.
ReplyDeletewatanzania wana mambo mengi ya msingi wanahitaji kutatuliwa kwa ajili ya maendeleo yao, uraia pacha hauna tija yoyote kwa maendeleo ya nchi hii. we ukipapenda mahali kuliko Tanzania hamia hukohuko undumi la kuwili wa nini
ReplyDeletenchi hii hakika haijielew na serikali yke kwa ujumla..katiba imewashinda na sasa wamehamia kwenye uraia pacha...shame on you government
ReplyDeleteNyie mnaojiita mnauwezo, mnataka uraia pacha, kisha mnali'chokonoa' mnakimbilia kwenye hizo nchi zenu pacha, mnatuacha sie wanyonge tunaumia... hasa wanasiasa, mnaanzisha vurugu na maandamano yasio na kichwa wala miguu, tupigwe nyie mkimbie, sisi tusio na uraia pacha inakulakwetu. Ukiona umechoka kuwa mtanzania, we badili uraia wako tu kama akina Masogange, hatutaki balaa.......Tanzania bila uraia pacha INAWEZEKANA.
ReplyDeleteKafie mbele wivu tu wa kimaendeleo ndio unaokusumbua sababu huna uwezo wa kuishi mamtoni, wewe kaa tu na hiyo bongo yako vumbi tupu mpaka kwenye kope, sisi huku saruji mpaka vichochoroni kula sana bata tomba sana akina dada wa kitasha pigiwa sana simu tukawatombe
Deleteww pimbi uctuletee siasa za kimihemko hapa! nchi ynywe ajira nanga za paa! majirani wnzetu kivumbi wanakiona kwa alshabab pamoja naufinyu wa ardhi walionao! na bado maendeleo hatujayaona! elimu bado mtihani huku! tulizana kwanza mpaka tukuambie nyani ww! naujue kuwa hatutaki utani na ardhi hii! kwani huko waliko ckuna uraia wa nchi mbili wachukue tu,ss tutawatambua tu hamna shida.
ReplyDeleteUnafirwa na baba yako
DeleteWatanzania tunaposhindwa kutatua jambo dogo kama hili la sheria ya uraia pacha, ni dhahiri kuwa mambo makubwa hatuyawezi. Sheria yoyote ya uraia huwa ina vigezo vyake; huwezi kuomba uraia pacha na kuupata bila kupimwa vigezo vinavyotakiwa kisheria. Jambo lililotakiwa kufanyika hapa katika kutunga sheria hiyo ni kweka vigezo vya msingi vinavyotakiwa kikamilishwa kabla mtu hajakubalia kuwa na uraia wa Tanzania na nchi nyingine. Aneyeshindwa vigezo hivyo, hata kama alizaliwa na kukulia Igunga lakini sasa anaishai London asiruhusiwe. Baada ya hapo tujadiliane vigezo hivyo, lakini leo kila mtu anakujwa na majibu ya jumla jumla tu kuonyesha kuwa hatuwezi kuangalia mambo kwa kina. Ndiyo maana hata mawaziri wetu husaini mikataba kijumla jumla bila kuisoma vifungu vyake.
ReplyDeletewahindi muliwapa nymba za natinal housing wenyewe,dunia nzima kila nchi ina mgeni ,marekani yenyewe wafanya kazi wengi ni wageni,chakufanya ni usimamizi,na safu ya ulinzi iliyo makini,kwa kushirikiana na watanzania walioko ndani na nje,hata kwenye biashara,mwingine amedai wasomi wako wa kutosha, huo ni upeo wa macho yako,ingekuwa hivyo msingetoka n jekusoma kuf,afanya mazoezi ya utabibu,ulaya,ni upeo mdogo wa kufikiri.
ReplyDeletepia ni laana kumkataa mtoto wako,damu yako ndicho kitakacho fuata Tanzania,umezaliwa ,Tanzania,ukosoma,bongo,mpaka chuo kikuu,,ukapata bahati ya kutoka nje,leo unaniambia,sio mtanzania?hapo ndio unaongeza uadui wala hujengi,mtu anaijua singida,km london,alafu unadai ,sio mzaliwa,angalieni vizuri,hata wanyama wana hama,na ndege,yaani miaka hii ya kuishi 70 mpaka 80 ukiwa na nguvu ndio inaleta ubaguzi wa rangi hivi,ok badi south afrika wangewafukuza wazungu,iila nashangaa waliwafukuza,wazimbabwe,
ReplyDelete