Yamoto Band inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi kufanya vizuri kila kukicha na hivi sasa wanatamba na ngoma tatu zikiwa ni pamoja na Nibemende/Nitajuta, Niseme.
Akiongea kupitia kipindic ha The Chart ya 100.5 Times Fm kinachoongozwa na Jayree, Asley ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema kuwa Said Fella (boss wao) amekuwa msaaada mkubwa katika nyimbo zao zote.
“Mara nyingi sisi huwa tunafanya melodies yeye anatoa maneno…Producer alitengeneza beat akatuita studio tukaanza melodies na maneno kidogo yetu. Bahati nzuri Mkubwa alikuwa anatoka kwake anakuja studio tukampigia simu ‘mkubwa sisi tumepata melody kuna nyimbo tulikuwa tunafanya hapa studio ila bado tunaona maneno kama hayajakuwa mazuri. Kweli mkubwa alivyokuja kuyasikiliza akaanza kuyapasua neno maoja baada ya moja.” Amesema Asley.
“Lakini maneno asilimia 90 ya nyimbo hiyo yote alitoa mkubwa. Na idea ya Nitajuta pia katupa baadhi ya maneno. Kama ukisikia sijui ‘mtu kunywakunywa milenda’ yote katoa yeye mkubwa Fella. Yaani mara nyingi yeye ndiye anatusaidia. Hii nyimbo ya mwisho yeye alitupa idea lakini maneno tulitoa wenyewe.” Amefafanua.
Wimbo wa Nitajuta wa Yamoto Band umeshika nafasi ya pili kwenye The Chart ya 100.5 Times Fm wiki hii.
Kipindi cha The Chart kinakuwa hewani kila Jumamosi kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saa sita kamili mchana. Unaweza kusikiliza online kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.
hii nyimbo .... huu wimbo?
ReplyDeleteWimbo huu au mwimbo huu, ndiyo sawa. Nyimbo ni zaidi ya mwimbo mmoja, kwa hiyo ni hizi nyimbo, siyo hii nyimbo
ReplyDeletenawapenda hawa watoyo wako serious na kazi na hata video zao ni nzuri na wasichana wanaoshuti nao pia ni warembo na wembamba.
ReplyDelete