Stori: Imelda Mtema
FAGIO! Mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amemmwagia sifa shosti yake Wema Sepetu na kudai anafaa kuwa mke kama alivyo yeye.
Akimmwagia sifa mbele ya kinasa sauti chetu, Aunt alisema Wema anajua mapenzi ya dhati, anajali, mcheshi na anajua maisha tofauti na watu wengi wanavyofikiria.
“Siyo kwamba namsifia lakini Wema anafaa kuwekwa ndani, unajua watu wanashindwa kujua tu kwamba Wema nje ya ustaa wake anajua kuhimili maisha, anafaa kuolewa,” alisema Aunt.
Wema na Diamond wapo katika mikakati ya kufunga ndoa.
Aunt Ezekiel Ampigia Debe Wema Sepetu Asema Anafaa Kuwa Mke Mwema
3
September 08, 2014
Tags
Nadhani kwa sasa magazeti yanawalipa,maana duuuuuuuuuuuuuuuuu.
ReplyDeleteHarusi ya uwanja wa Taifa,hakuna kuzamia.twasubiri.
ReplyDeleteMwanamke anafa kuolewa hapigiwi debe kwani biashara ya samaki
ReplyDelete