Polisi nchini Uingereza wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio ambalo mshambulizi kutoka nchini Italia na klabu ya Liverpool Super Mario Balotelli alitukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Polisi katika mji wa Merseyside wameanzisha uchunguzi kufuatia matusi hayo yaliyotokea baada ya mshambulizi huyo wa Liverpool kutuma ujumbe akiicheka kichapo cha Manchester United mikononi mwa timu ndogo ya Leicester siku ya jumapili.
Baloteli aliandika ''Man Utd...LOL'' na ujumbe wake ukasambazwa zaidi ya mara 150,000 na mashabiki wake.
Hata hivyo miongoni mwa mwa wale waliouona ujumbe huo walimfokea kwa kuicheka United na wakamtusi kwa msingi wa rangi yake.
Japo ni raiya wa Italia, Balotelli mwenye umri wa miaka 24 ana asili ya kiafrika.
Polisi tayari wamefunga kurasa kadha zilizotuma jumbe hizo huku wakianza uchunguzi waliozimiliki ni kina nani na wanaishi wapi iliwakamatwe na kujibu mashataka ya ubaguzi wa rangi.
Kundi linalopigania kumaliza ubaguzi wa rangi katika michezo Kick It Out lilisema kuwa baada ya kuarifiwa kuwepo kwa matusi yenye kumdhalilisha Balotelli, kundi hilo lilianzisha uchunguzi kwa ushirikiano na polisi wa mitandao ya kijamii.
Sio mara ya kwanza kwa mshambuliaji huyo kudhulumiwa kwa misingi ya rangi yake.
Balotelli ambaye alikuwa uwanjani Liverpool ilipobamizwa mabao matatu kwa moja dhidi ya West Ham mwishoni mwa juma lililopita amewahi kudhulumiwa kwa misingi ya rangi yake wakati timu ya Italia ilipokuwa ikijifua kwa ajili ya fainali za kombe la dunia mwezi mei mwaka huu .
Awali pia aliwahi kutukanwa akiwa klabu za Inter Milan na AC Milan zote za nchini kwao Italia.
USIJALI BALOTELLI. MTI WENYE MATUNDA MARA ZOTE NDIO UNAPIGWA MAWE!!!
ReplyDelete