Pendekezo la Rasimu ya Katiba kuwa wabunge walau wawe na elimu ya kidato cha nne limetupiliwa mbali na wajumbe wa Bunge Maalumu, baada ya Kamati karibu zote kulikataa.
Kamati hizo zimependekeza kigezo cha elimu kuanzia walau kidato cha nne kama sharti muhimu la mtu anayetaka kugombea Ubunge kiondolewe, badala yake mgombea ama ajue tu kusoma na kuandika, au ajue kusoma na kuandika Lugha ya Kiswahili au Kiingereza kama ilivyo kwenye Katiba ya sasa.Mbali na pendekezo hilo, kamati hizo zimegawanyika kuhusu Ibara ya 129 ya Rasimu ya Katiba inayowapa wananchi nguvu ya kumuondoa mbunge wao madarakani kabla ya miaka mitano kumalizika.
AIBUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU
ReplyDeleteama kweli, sayansi na teke ulimwengu huu bado mna mambo ya kizamani! kwanini tunapeleka watoto shule? nani atakuwa mwakilishi wetu kimataifa kama mnatetea upuuzi wa mbunge asiwe na elimu ya juu? kujua kusoma na kuandika sawa, ila dunia ya sasa siyo ya enzi za mwalimu, ukiwa na elimu ni rahis kujenga hoja, katika vikao vya kimataifa. ila sishangai, ukitaka kikao kuendesha kikao na kisiwe na maswali mengi au hoja endesha kwa kiingereza, na kama ni kiswahili utaona kasheshe za maswali! mtazamo wangu mwenye elimu ataongoza siasa kielimu sio siasa za blaa blaa. mfano, unamteua Waziri wa nishati na madini anaejua kuandika na kusoma tu, ataongoza asichokijua? je, waziri magufuri angekuwa anajua kusoma na kuandika tu, barabara zetu na madaraja angekuwa ndiyo tu, hata wakivurunda wakandarasi! Wabunge twende na wakati na Tanzania yetu. dunia ni uelewa siyo mbumbumbu!
ReplyDeleteKweli ni aibu mdau hapo juu,Ikumbukwe katiba ya sasa imetungwa lini? ni kipindi ambacho darasa la saba aliweza kupata kazi ya maana,ofisi yoyote bila wasiwasi,leo darasa la saba anaweza kuajiriwa?
ReplyDeletekwanza nimuombee baba wa Taifa mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amina. aliliona hili mapema suala la elimu, ndiyo maana akaleta elimu ya watu wazima. maana alijua Taifa la watu mbumbumbu ni sawa na bure. maana yake ni nini, Mwalimu alikuwa na elimu ndiyo maana aliweza kupigana na maadui. hivi kweli karne hii watu wanadigree, wewe unaewaongoza unajua kusoma na kuandika, kweli utaongoza! tatizo siasa nyingi, pasipo maarifa, waziri wa Elimu kasoma elimu ya watu wazima, kaimu wake ana degree, kalabagao! haya majanga kweli kweli, tuache siasa za blaablaa, twende na wakati!
ReplyDeleteYaani hii nchi tunakoelekea sasa sijui wapi jamani,
ReplyDeletesasa vyuo na shule za sekondari ni vya nini kama kiongozi au msemaji wa wananchi hana lazima ya elimu ya chuo,kumbe kama ni kusoma na kuandika tu si ndio kusema wote tuishie shule za msingi tu?Yalaaaaaaaaa,TZ tutachekwa mpaka basi.
Ruska tu ila akishashinda ubunge ahakikishe anajiendeleza kielimu.Nchi hii inaendeshwa kidemokrasia kila mmoja ana haki ya kupata nafasi ya uongozi ili mradi tu taratibu ziwe zimefuatwa.Hata baadhi ya hao viongozi wenye elimu ya juu tunaona jinsi utendaji wao na utekelezaji majukumu unavyotia shaka.Kwanza wataamu wa uongozi wanasema kiongozi si lazima awe na akili sana isipokuwa wasaidizi wake ndiyo wanapaswa kuwa na elimu kubwa.So guys let's be realistic........... Instead of analyzing issues based on our emotions .Viva Tanzania!
ReplyDeleteTamaa tu za madaraka... mbona hao darasa la 7 wakimaliza shule hawaajiriwi... Ni Aibu kwa wabunge wenyewe na kwa taifa Zima..!!!1
ReplyDelete