Neema inazidi kumuangia Diamond Platinumz na leo amepata habari njema baada ya kutajwa kuwania tuzo ya MTV EMAs huku akipokea tuzo kutoka nchini Australia.
Diamond amewapa mashabiki wake habari njema za ushindi wa tuzo ya AAMA ya Australia kupitia tiketi ya collabo ya aliyopewa na Desert Eagle, wimbo unaoitwa ‘Everyday’.
“Ningependa niwajulishe kuwa kijana wenu nimepata tunzo nyingine toka Australia ya Collabo bora ya Mwaka toka kwenye tunzo za #AAMMA_Awards kupitia nyimbo niliyoshirikishwa na Desert Eagle iitwayo #EVERYDAY..... (jus wanted to inform you that, your favourite artist @Diamondplatnunz won another award from Australia on #AAMMA_Awards as best Collaboration song of the Year..).” Ameandika.
Wakati huo huo, mtoto wa Tandale ametajwa kuwa moja kati ya wasanii wanaowania MTV Europe Music Awards mwaka huu huku akichuana na wakali wengine kutoka Afrika akiwemo Davido, Toofan (Togo) na Goldfish (Afrika Kusini).
Msanii mwingine wa tano akisubiria kutajwa baada ya mashabiki kumpekeza kutoka kwenye kundi la wasanii sita ambao ni Anselmo Ralph, Gangs of Ballet, Mafikizolo, Sarkodie, Sauti Sol na Tiwa Savage.
Aidha, majina yote ya wasanii wanaowania tuzo hizo yatatajwa September 16 ambapo upigaji kura utaanza rasmi.
Hongera Diamond Platinumz, Tanzania inazidi kutajwa kwenye majukwaa ya kimataifa.
Hivi anatumia lugha ganii ya mawasiliano. Na hawa wazungu?maana alivyokuwa anafanya inter view na karrueche I felt bad,kingereza chake ni hatari,dai unahela bwana kwanini usichukue kozi ya kiingereza?
ReplyDeleteaarrrgghh wacha kasumba wewe kiengereza ni nini nafanya kazi na white people wanotoka bara ulaya na kiengereza broken na walaaaa hawajisikii vibaya na tunaona kawaida tena ukute mtaliaono bora ajifunze kiswahili kuliko icho kiengereza chako bora cha kuombea maji ata ivo diamond katoka mbali na lugha wacha tantarira mpe hongera zake
ReplyDeletehahahhahaaaaaaaaaaa kiingereza ni lugha tu kama mimi ninavyokijua kichaga changu acha kupaisha lugha za watu. dai hajazaliwa na hicho kiingereza ukitaka msemeshe kikwao ndio utatambua uwezo wake wa lugha. wazungu wenyewe kiswahili hola sasa wapi na wapi bannnnaaaaaa
ReplyDeleteSasa Huku nchi za ulaya anatutia aibu,nchi yetu inaonekana ovyooo,watu tunaonekana atujasoma.
ReplyDeletedai ongera san kujua kigereza na kutojuz aijalisho mbona fally ipupa ni msaninii mkubwa.na ajui lugha ya kingerereza acheni ukoloni ban
ReplyDeleteEnglish lungha tu bro sio kila anaongea English ndio ana elimu kuna British wengi tu wanaongea coz ndio lugha yao lakini hata kusoma hawajuwi
ReplyDeleteHongera sana......lkn naomba kuuliza kwa nn ukiwa jukwaani hadi uvue nguo?siingilii maisha yako lkn nami ni mmoja wa wadau wako naomba kujua..lkn kama itakua tabu kujibu c mbaya ukanipotezea....
ReplyDelete