Diamond Platnumz Azungumza Kwa Mara ya Kwanza Mambo Sita Kuhusu Fujo Zilizotokea Ujerumani

Kuanzia siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye kiwanda cha burudani Tanzania imehusu fujo zilizotokea Ujerumani kwenye show aliyokwenda kufanya Diamond Platnumz huko Stuttgart.
Kilichotokea ni kwamba saa kumi alfajiri ndio promota alimpeleka Diamond kwenye ukumbi kunakofanyika show. Kwa nini ilitokea akamchelewesha? nini kilitokea baadae? hizi hapa chini ni kauli za Diamond mwenyewe kwenye exclusive na millardayo.com

1. ‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo lilikua ni hela, balance iliyokua imebaki ni balance ndogo kama EURO 3500 hivi ambazo ni zaidi ya milioni 7 za Tanzania, ninavyojua Mapromoter wengi wa nje wakifanya show huwa wanauza na vinywaji wenyewe na wanapata hela nyingi sana kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so nahisi labda walivuta muda ili waendelee kuuza vinywaji zaidi’

2. ‘Walichelewa kunipeleka kwenye show, walinifata kwenye mida ya saa tisa usiku na wakawa hawana hela yangu iliyobaki, nikawaambia siendi kokote mpaka wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500 wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio tukaenda kwenye show’

3. ‘Tukafika kwenye show saa10 kasoro, kweli hata ningekua mimi shabiki ningekasirika ningefanya vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja na wametoka kwenye miji na nchi jirani, niliwaambia wanipeleke nikafanye show ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi sana nje lakini Mapromota walikua waogawaoga kunipeleka ndani’

4. ‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje, nikamwambia promota atupeleke ndani tungefika kwenye stage ingetulia baada ya sisi kuimba manake ni vitu tunakutana navyo kwenye muziki lakini promota walikua waogawaoga, askari wa Ujerumani karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti ukawa mkubwa’

5. ‘So dakika ya mwisho tukaona hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini, kiukweli nimesikitishwa sana manake nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart, imenisikitisha manake watu walikua kuniona alafu mwisho ikashindikana kuwafikishia walichokitarajia’

6. ‘Nafikiri October tutakua na show nyingine na itafanyika kulekule, nilikua nazungumza na uongozi wangu kwamba wanataka show nyingine na tayari wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’
Unaweza kumsikiliza Diamond mwenyewe kwa kubonyeza play hapa chini.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa bongo unatulingiaga na unajipa promo bila mil 50 na kuendelea hupandi jukwaani wakati hao wametaka kukuua kwa mil 14 tu... tena nchi za watu ambazo kwa upeo wangu nahic ungehitaji mkwanja mrefu zaid.. me naamin kuna kinachokupatia hela zaid nyuma ya pazia sio huo mziki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeona eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh

      Delete
  2. Na yeye ndio atajua umuhimu wa time Kwani sio Mara ya kwanza kuchekewa kufika kwenye show nafikiri ushapata somo next time jali wakati hujawa star bado ole wako hukuchezea kichapo

    ReplyDelete
  3. Mdau nakupenda bureeeeee wanatudanganyadangaya mabwegeee,nchi za ulaya hela anayopewa n nusu ya hela anayopata bongo akipiga show.kuna njia mbadala za kumuingizia hela,endeleeni kudanganywa,

    ReplyDelete
  4. Mi nahisi kuna kitu anasafirisha.

    ReplyDelete
  5. ajiangaalie atakuja aibika!!!!

    ReplyDelete
  6. Diamond wanaivaa na kinje alivyotimuliwa ujerumani akakimbilia south kwa kinje.

    ReplyDelete
  7. Mi tangu amdhalilishe Demu wake kanitokaAaa,na demu ndo kashapenda,aoni wala asikii ushauri Wa mtu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad