Jack Patrick Atuma Ujumbe Mzito Kwa Watanzania Huku Akiwa Gerezani China

Stori: Imelda Mtema
MWANAMITINDO wa Bongo aliyepo nyuma ya nondo huko Macau, Hong Kong nchini China akitumikia kifungo cha miaka sita baada ya kukutwa na hatia ya kubeba madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ ametuma ujumbe mzito kwa mashabiki wake.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, rafiki wa karibu wa Jack ambaye hakupenda jina lichorwe gazetini, alisema kwamba mwanamitindo huyo amekuwa akimuandikia barua mara kwa mara lakini safari hii ametaka ujumbe wake uwafikie Watanzania.

“Amesema watu wasimhurumie kuhusu kufungwa, amesisitiza sana juu ya suala mavazi na mitindo. Amesema hapendi kuona Tanzania inayumba katika masuala ya mitindo ambayo yeye alikuwa akiiamini kwamba ni kazi ambayo inaweza kuwaingizia kipato watu wengi,” alisema rafiki huyo wa karibu.

Rafiki huyo alizidi kuweka wazi kuwa mara nyingi Jack hapendi kuwaambia juu ya maisha ya jela kwani hapendi kabisa kuwapa watu simanzi bali anapenda watu wajue anaishi maisha ya kawaida.
“Mara nyingi Jack hapendi kabisa kueleza maisha ya jela, hapendi kuwaumiza wat, anachopenda ni kujua nini kinachoendelea katika fasheni,” alisema rafiki huyo wa Jack.

Rafiki huyo alisema kuwa Jack bado anaagiza nguo ambazo alikuwa akipenda kuvaa hasa lineni nyeupe na kuwataka watu wahisi kama yupo masomoni na atarejea tu akiwa salama.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea Bangkok, Thailand kuelekea Guangzhou, China.
GPL

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yani me story iandikwe na uyo imelda wa global arrrggh ata sijishuhulishi kusoma najua ni uwongo tu yani awa ndo type ya wandishi wanatungaa story ili wale kindy ya wanafiki na wachonganishi hawanaga ukute ata iyo story kapanga tu ili apate commission kazini kwake mfyuuuuu

    ReplyDelete
  2. yaan ata mimi nilikua namkubali sana Imelda ila kwasasa nimeshaanza kumchoka kwa story zake feki hajui kama anajiharibia

    ReplyDelete
  3. Kiroho safi tu udaku gaya mapic yako yanageuka geuka sijui maandishi yanapanda na kushuka hyavutii afu yanachosha tu yan hap hujabun kitu zaidi unatuumiza macho yetu tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad