Jaji Warioba: Bunge lisitishwe Katiba Mpya Haiwezi Patikana Ndani ya Wiki Mbili zilizobakia

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema ni vyema Bunge Maalumu la Katiba likasitishwa kwani Katiba bora haiwezi kupatikana kwa muda wa wiki mbili.

Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku moja baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kumtaka Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kulisitisha, huku mwenyewe akisema litaendelea na hadi kufikia Oktoba 4 Katiba inayopendekezwa itapatikana.

Jaji Warioba alieleza kushangazwa kwa haraka waliyokuwanayo wajumbe wa Bunge hilo 

wakati wanajua kuwa Katiba haiwezi kupatikana kwa muda uliobaki.

Alisema wiki mbili au tatu zilizobaki ni chache mno na kwamba Katiba mpya haiwezi kupatikana, hivyo ni vyema sasa busara ikatumika kulisitisha.

“Mimi sizungumzii kauli ya Ukawa, lakini natoa maoni yangu kwamba sidhani kama watamaliza kwa kipindi hiki kifupi, kuna mambo hawawezi kupata kwa muda huu mfupi.

“Ninachotaka watumie tu busara waliahirishe… sijui haraka yao hii ni ya nini. Kwanini wanashindwa kuelewa kuwa Katiba ni suala la maridhiano?” alihoji Jaji Warioba.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee wetu, siyo kwamba wana haraka au wanajua wanachofanya ila tu ni ulafi na matumbo yao ndiyo wanajali, in two weeks watakuwa wameingiza kiasa cha milioni za kutosha kwakila mmoja!!

    ReplyDelete
  2. Zee la kunywa gongo limeishiwa sera,angalia hata marehem Ongara alimuimba katika wimbo wa Niseme nini!
    Wengine wanalalamika hivi sasa,wamesahau madhambi yao,walipewa madaraka wakalala usingiizi,tembo wanateketea.Saa mbili asubuhi foleni kwenye gongo ofisi ipo nananii weee,aibu!

    ReplyDelete
  3. wewe fisadi hapo juu acha kumtukana mzee wetu, hawa ndiyo walikuwa watu wenye maadili enzi zao, ndiyo walioiweka hii nchi sawa, SALUTE kubwa Mzee Warioba, sio hawa wa sasa hivi kazi kuuuuuulaaa tu!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad