FEDHA mwanaharamu! Katika hali ya kushangaza, staa wa filamu ambaye fedha imemtembelea kwa sasa, Kajala Masanja ‘K’ amenaswa akimwaga fedha kama amechanganyikiwa mbele ya kadamnasi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilitokea hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo muigizaji huyo alionesha jeuri ya fedha baada ya kupagawishwa na sebene la Yamoto Band.
ALIINGIA NA WAPAMBE
Awali, paparazi wetu alimshuhudia Kajala akitinga viwanjani hapo akiwa ameongozana na wapambe takriban 15 na kwenda kukaa katika meza moja ambapo mhudumu aliwasikiliza kujua wanachokunywa.
VINYWAJI VYAAGIZWA NJE
Kutokana na uzinduzi huo kutokuwa na pombe, K aliamuru kila mtu aletewe kile anachokihitaji halafu bili yote apelekewe yeye, Mama la Mama kama wanavyowaita watoto wa mjini.
“Waletee hawa vinywaji wanavyojisikia kunywa pia wasikilize meza ile pale kisha bili niletee mimi,” alisikika Kajala
MINONG’ONO YAMTIA WAZIMU
Baada ya kauli ile wafuatiliaji wa mambo ya watu hasa wakienda shughulini wakaanza kutoa minong’ono kuwa hata iweje bado Kajala hajafikia uchezeaji wa fedha kama alivyokuwa shosti wake wa ‘long time’, Wema Sepetu aliyepewa taito ya Madam kutokana na kujua kuzitumbua fedha.
“Kwani kuagizia watu vinywaji ndiyo kuonyesha kufuru au jeuri ya fedha, angalia wahudumu wanavyogawa vinywaji kwa kusuasua, unafikiri angekuwa Madam (Wema) angekubali hata akae muda wote asiende kutunza thubutu, chezea Madame (Madam) wewe,” alisikika mualikwa mmoja.
YAMOTO BAND WAMWINUA
Ndani ya muda mfupi, Kajala akavunja ukimya baada ya bendi ya Yamoto kupiga wimbo wa Nitajuta ndipo Kajala aliposhindwa kuvumilia na kwenda kuwamwagia fedha huku wapambe wake wakimshangilia.
“Ndiooo mkurugenzi hivyo ndivyo ujana unavyoliwa,” kelele zilisikika kutoka katika meza waliyokuwa wameketi wapambe wake.
KAMA LAKI SITA NA USHEE
Ufukunyuzi wa paparazi wetu kwa harakaharaka, ulizihesabu fedha hizo alizowamwagia watoto hao wa Mkubwa Fella ambapo hesabu zilionesha zilikuwa zaidi ya shilingi laki sita.
AKOSOLEWA
Hata hivyo kuna baadhi ya watu walimkosoa staa huyo kwa kusema kitendo cha yeye kupata fedha kwa sasa kinaonekana kumchanganya kiasi cha kuzimwaga pasipo kuwa na sababu ya msingi.
“Bora angetunza kidogo na nyingine akatumia kwa vitu vya maana likiwemo suala la kumsaidia mume wake ambaye yuko jela kwa kushindwa kulipa faini ya shilingi mil. 200,” alisikika mdau mmoja wa filamu ambaye hakutaka kuanikwa jina gazetini.
UZALENDO WAMSHINDA STEVE NYERERE
Kadri Kajala alivyozidi kumwaga fedha, uzalendo ulimshinda Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambapo alimfuata Kajala na kutaka na yeye amtunze.
“Hebu kuwa na adabu, mi mkubwa wako na mimi nitunze kwanza mambo mengine yaendelee, haiwezekani uoneshe jeuri ya fedha kiasi hiki wakati mimi mdau nipo hapa hunipozi,” alisikika Steve Nyerere.
AMEZIPATA WAPI FEDHA?
Baada ya vurugu zote zile kufanyika, paparazi wetu alimvaa Kajala na kutaka kujua vyanzo vya fedha hizo na kumuuliza kama amehongwa, akachomoa.
“Mimi sihongwi ukitegemea fedha za mwanaume huwezi kuwa na heshima mjini, nina biashara zangu na kampuni yangu hiki ninachokitumia hapa ni faida tu ya siku mbili tatu mimi mjasiriamali wewe,” alisema Kajala.
TUJIKUMBUSHE
Kumbukumbu zinaonesha, kipindi ambacho Kajala na Wema walikuwa marafiki, Kajala hakuwa na fedha nyingi lakini baada ya kutofautiana, pesa imemtembelea huku mwenzake akidaiwa kuyumba kiuchumi.
GPL
Kajala Azuzuliwa na Pesa, Afanya Vituko ,Amwaga Malaki Uwanjani
14
September 10, 2014
Tags
Hivi wewe muandishi ni mnafikiiiii huwezi andika stori mpaka umuingize Wema?basi Kama unataka wakosane awakosaniiiii mngese wewe,uchocheziiiiiiiiiiiiiiii we vipiiiiiii????????
ReplyDeleteKweli huyu muandishi ni mfitini,mchochezi,na anaonyesha kabisa kuwa ugomvi wa Wema na Kajala anaushabikia sana.Lakini hata wewe mdau umeonyesha ni team Wema kabisa,kwani mpaka utukane?
Deletehawa waandishi shule hawana ...mengi wanayoandika ni uwongo na uchochezi ... hebu wawaache watoto wa watu wanataka watu washindwe kuzikana kwa mambo yao ya uzushi ... ss hapo Wema kaingizwaje si ndo kukosa point ya msingi .....ila Wema na Kajala make mkijua waandishi hawana shule hivyo ili waweze kupromote story zao inabidi wawaweke nynyi kwa mema au mabaya immladi wauze so kuweni makin mistake kugombana wote ni mabint wazuri then mlisha kuwa mabest friend haina haja ya kuzalilishana ..... mmm nawapenda wote mnavyogombana mnaniumiza sana
ReplyDeletenakushauri kay achana na starehe zisizo mwisho jifunzie alipokesea ex shosty wako haipendezi mwakani tusome story za kay kafulia kama madame kuweni serious na matumizi ya hela tena wewe uko na mwana anazihitaji zaid hela tena kaa low profile itakusaidia zaid ukitokea kwenye media iwe kikazi zaid na si starehe mwaya utafika mbali showing off haisaidii ungekuwa na hela asaa ungemtolea mume wako atoke jela ata kama akitoka kila mtu ashike hamsini zake
ReplyDeleteMdau una akili mpaka zinapitiliza,
DeleteKay huu sio wakati wa kuonyeshana jeuri ya fedha,umri umeshaenda,una mtoto
na mbona hatusikii unatengeneza mjengo sehemu fulani?badala yake eti unaonyesha jeuri ya pesa kutunza watu na kuwapa offer zisizo za lazima,kwa nini hamjifunzi?
Sijui na mimi nikipata pesa nitakuwa mwehu kama hivi,mweeeeeeeeeee !
ReplyDeletepesa nitembeleeeee basi na mimi nione uzuri wako.
hivi hao wanaosema atoe millioni 200 wanadhani ni ndogo?? wasanii wenyewe wnapata milioni moja moja mnazuzuka na show off zao mkidhani wana hela!!
ReplyDeleteNamshauri apunguze starehe atakama anafanya sio kwa kujionesha kamahivi. Pili punguza wapambe sio watu wazuri kabisa wanakutumia ukishafulia wao ndio wa kwanza kukucheka na kukuona huna akili.
ReplyDeleteTuingie kwenye dini yao tutakua kama diamond na kajala na wengine jamani msishangae saaanaa kawaida tu
ReplyDeleteInashangaza sana mama wa mtoto mmoja tena ni independent mother anafanya ujinga kama huo. Hv wewe kajala kwenu huna ndugu wa kuwasaidia au ndio umetokea ukoo wa matajiri? Hizo hela si ungeenda kumuanzishia ndugu yako hata mradi wa kutengeneza sabuni za maji/unga au hata biashara ya kupika mikate akaingiza. Kweli maskini akipata, matako hulia mbwata. Unatia kinyaa.
ReplyDeleteHuyunae nisikio lakufa acha ajishaue simshauri chochote kamahela zake amwage ahonge atajaza mwenyewe walikuwepo kina jaq pemba kufuru zakutosha now wakowapi kajambe kulee
ReplyDeleteningependa sana kuona mtu aamue kuwaapa maskin vilema waonjwa alipe na ada za watu shule za msingi secinar vyuo nakuwapatia kila binadam kaz ndoningeamin unajeur yapesa achen dhambi mtaishia pabaya mkipata mnajishauwa mkikosa mnamlilia mungu wiz mtupu
ReplyDeletekajala hizo pesa si ungepeleka kanisani sadaka, unakumbuka ulivyotoka selo ndipo ulipokimbilia??? leo umesahau unatumia na wapumbavu wenzako
ReplyDeletewenye pesa huwa hawajishaui. visenti hivyo sifa za kijinga tu
ReplyDelete