Sikuwahi kupima HIV mpaka siku nilipoamua kwenda kupima tena baada ya hofu iliyotokana na maneno maneno ya watu waliolenga kuniondoa kwenye reli.
MAIN TOPIC.
Kwa kuwa tayari hofu ilijengeka ndani yangu.
Niliamua LIWALO NA LIWE. Taratibu nikapanda gari kwenda angaza, mbali kidogo na nikaapo.
Niliposhuka kwa gari nikachukua bodaboda. Nikamwambia jamaa"nipeleke angaza" jamaa akashituka na kuniuliza unaenda kupima UKIMWI?
Jibu langu"NDIO"
Jamaa "una moyo, mimi sipimi ng'o, kwa nini nijipe presha?"jamaa akanichukua huyo mpaka angaza.
Pale si mchezo, nikakuta watu wote kimya hadi wanatia huruma.
Tukasubiria huku tukiangalia filamu ya ukimwi,mara mhusika huyu.
Swali lake"nyie wote si mmekuja kupima UKIMWI?"
Jibu letu"NDIYO".
Yakapita maswali na maelezo mbalimbali kuhusu UKIMWI, mioyo ya wengi ilionekana kujaa hofu na yenye kukosa matumaini, watu tulikuwa watulivu mithili ya mtu anayesali kimoyomoyo, nyuso hazina matumaini, tukapima na majibu kwa kila mtu ni siri.
JAMANI KULE SI MCHEZO
Kupima Ukimwi si Mchezo, Jeuri na Ujanja Wote Mfukoni
2
September 20, 2014
Tags
Wewe fala unaogopa kupima miwaya karne hii? Miaka ya tisini ingekuwaje? kauzu mkubwa wewe!
ReplyDeleteWewe wa wapi?Kwani ukimwi dunia ya leo watu wanapima wenyewe majumbani,
Deletekwa nini ukafie Angaza kwa presha?