Mkubwa wa kazi ambaye amewahi kushika nafasi kubwa za uongozi katika taifa hili na mwenye kasi ya ajabu katika medani za siasa, uchumi katika chama chake, amekuwa akiwaonya wapinzani wake kutotumia kete ya mali zake kama njia ya kumchafua ki siasa.
Amesema hapendezwi na hilo, na jambo hilo halina tija kwa siasa zetu za Tanzania, kuna mijadala mingi ya ki taifa ya kujadili kwa maendeleo yetu na siyo mali zake kwani anazo mali za kawaida kuliko inavyozushwa.
Kakazia kwamba wapinzani wake wasijikite katika mali zake kwani "ALIYEPATA AMEPATA".
Haya wadau hizi ndiyo siasa za bongo watu wamewekeza kwenye kuchafuana tu. Chama cha CCM kazi ipo.
wewe ndiye rais mtaraajiwa!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeletehawana jipya tunajua wote hao hawana kiwango wanajisumbua we ndio rais mtarajiwa.
ReplyDelete