Man Walter Aeleza Walipofikia Katika Kufanya Kazi na 20 Percent

Mtayarishaji wa muziki kutoka Combination Sound, Man Walter aliwahi kutangaza kumaliza tofauti kati yake na 20 Percent aliyewahi kufanya vizuri kupitia mikono yake na kwa pamoja wakaeleza mpango wa kufanya mradi mpya.

Man Water ameongea na tovuti ya Times Fm na kueleza walipofikia baada ya ukimya wa muda mrefu tangu walipotangaza hatua hiyo.

“Off Course kwa sasa siwezi kuongelea sana kwa sababu wazo lilienda vizuri lakini nadhani kuna vitu viwili vitatu vilikwama, sijapata tena mawasiliano mazuri na 20. Labda tuvute subira tu, kwa sababu kama watu wana lengo la kufanya jema litakuwa tu…nadhani tuvute subira kwake.” Man Walter ameiambia tovuti ya Times Fm
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ukivumiliaaa mbele kweupe, 20% comeback aisee .Sauti na jumbe zako ni za kipekee

    ReplyDelete
  2. 20 naweza kusema ni star bora kwangu, kwanza alipata umaarufu Sana lkn hakujikweza, pili upatikanaji wake mtaani unasemekana kuwa adimu Sana, tatu hachagui aina ya watu wa kuongea nao, yani kwa kifupi ni wa pekee Sana, hizo tofauti nyingine ni human error tu hata mtu mwingine anazo, lkn rudi ufanye kazi bana 20 tunamisi sana maujumbe yako yaliojaa hekima na ucheshi ndani yake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad