Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Amewalazimisha Waalimu Kuchangia Jumla ya Shilingi 48,000/= Bila idhini yao

Katika hali isiyo ya kawaida, mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani Bwana Limbakisye Shimwela amewalazimisha waalimu wa manispaa hiyo kuchangia jumla ya Shilingi 48,000/= bila idhini yao kwaajili ya
1. Fulana alizowagawia kipindi cha mwenge, ambazo hata hivyo hawakuambiwa wala kukubaliana kuwa zitalipiwa.
2. Mchango wa elimu ambapo hakutoa mrejesho wa mapato na matumizi kwa mchango wa mwaka jana.
3. Mchango wa ujenzi wa maabara ambapo hakuwashirikisha katika kupanga kiwango
cha kuchangia.
Aidha ufafanuzi wa michango hiyo ni kwamba 13,000/= Ni fedha kwaajili ya fulana na kofia, 5,000/= mchango wa maendeleo ya elimu na 30,000/= kama mchango wa ujenzi wa maabara katika shule za sekondari. Suala hilo limeibua maswali mengi kwani walengwa hawakuitwa ili kukubaliana kwa pamoja kuhusu michango hiyo.
Ikumbukwe kuwa miezi michache iliyopita mkurugenzi huyu alitoa barua zilizojaa vitisho kwa waalimu ambao hawakwenda kukesha katika viwanja vya shule ya sekondari Umoja na waliokesha hawakulipwa chochote kama sheria inavyotaka kwamaana tukio hilo lilifanyika muda ambao si wakazi.
Waalimu wengi wamevunjika moyo kutokana na vitisho na matamko ya mara kwa mara ya mkurugenzi huyo hasa yale yanayohusu michango ambayo hata hivyo hawahusishwi katika makubaliano.
Licha ya barua za kuwataka waalimu wasiolala kwenye mwenge kutoa maelezo, Mkurugenzi huyo amewaandikia barua walimu ambao hawajatoa mchango wa fulana na kofia kuwa wanatakiwa kufanya hivyo mapema kwani walikopeshwa fulana hizo japo hakuna vielelezo vinavyo thibitisha hayo.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe unategemea mkurugenzi afanye nini wakati raisi Kikwete ameagiza ifikapo mwezi november mwaka huu kila shule ya sekondari iwe na maabara ya kisasa yenye vifaa bila kueleza fedha hizo zitoke wapi......mwisho wa siku wakurugenzi wa halmashauri wanaangalia wanyonge wao wako wapi na wanaona ng'ombe wa kumkamua hata ikibidi damu ni walimu maana ndio wengi kwenye halmashauri na pia hawana pa kusemea wala hawajui kulalamika ilhali wanaidai serikali mabilioni ya fedha zao.......hapa ndipo serikali ya ccm ilipotufikisha watanzania........kwamba wenye fedha hawalipi kodi na serikali haihangaiki kukusanya kodi toka kwa wafanyabiashara wakubwa ila wanabaki kuwaongezea mzigo kila siku wafanyakazi simply kwa sababu wanaweza ti kukata moja kwa moja bila wafanyakazi kukataa.huu ni wizi wa wazi wazi mchana kweupe........walimu na wafanyakazi wengine tusimame kidete kukataa udhalimu na wizi huu ws serikali......njia pekee iliyobaki ni kuwanyima ccm kura kwenye uchaguzi maana njia nyingine zote zilizo kwenye katiba kama migomo na maandamano ya kudai haki zetu wameshaziua kwa kutumia polisi na mahakama ambao bado tunawalipa kwa kodi zetu........kazi kwenu wafanyakazi kuamua kusuka ama kunyoa na ukombozi wenu ninyi walimu na wsfanyakazi wengine uko mikononi mwenu sasa

    ReplyDelete
  2. tatizo sisi watu wa kusini na mimi nikiwa mmoja wapo tunapenda kulalamika nani atatuletea maendeleo shule hazina maabala na madawati ukombozi ni sasa na upo mikononi mwetu

    ReplyDelete
  3. kuchangia unyago hata hatulalamiki sherehe kubwa kuwafundisha watoto kukata mauno wakati elimu hatuchangii tunachangishana hadi bac baba wa watu afanyeje?

    ReplyDelete
  4. bhaaa bwana wewe kuninogea wewe? nakupendaje ntonto nzuri?

    ReplyDelete
  5. sasa kama kuchangia si wachangie wananchi wote kwanini iwe walimu peke yao.......!? achen upumbavu nyie Anonymous 8:55 & 9:00

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad