Nyerere Alikumbuka Shuka Wakati Kumekucha Juu ya Umuhimu wa Mfumo wa Vyama Vingi Nchini

Kuua mfumo wa vyama vingi miaka ya 60 na baadae kuiacha ya CCM itawale bila uwepo wa vyama vya upinzani lilikuwa ni kosa kubwa sana la utawala wa awamu ya kwanza na matokeo yake watanzania wengi walizoea mfumo wa vyama vingi na ndio sababu kubwa ya watanzania wengi kuukataa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Pamoja na Nyrere kushauri mfumo wa vyama vingi uanzishwe licha ya zaidi ya asilimia 80 ya watanzania kukataa mfumo huo,ilikuwa ni hatua iliyochelewa mno kwani teyari mfumo wa chama kimoja ulishaota mizizi na ulishatutia hasara kubwa mno watanzania kwani chama tawala kilikuwa hakina mpinzani na hivyo walifanya waliyotaka bila ya hofu yoyote tofauti na sasa ambapo "pressure" ya upinzani inasaidia kui-shape serikali iliyoko madarakani.

Hivi umewahi kujiuliza maendeleo ya nchi yetu yangekuwaje leo kama tungeendelea kuwa na mfumo wa vyama vingi tangu uhuru.Ule utaratibu wa kupiga kura kuchagua kati ya picha ya mtu na kivuli hukupaswa kuwepo kwa muda wote ule.

Maswali ambayo huwa najiuliza ni kuwa Mwalimu Nyere allitaka atawale pasipo upinzani(misukosuko) au aliona upinzani hauna umuhimu kwa wakati ule au alikuja kujua umuhimu wa upinzani baada ya yeye kutoka madarakani na kuona mambo yanaenda hovyo?Je,ni kweli mfumo huu ulipata msukumo kwasababu ya shinikizo la kimataifa?Na kama ndio,je shinikizo hilo halikuwepo kabla ya hiyo miaka ya 90 na kama lilikuwepo mbona lilipuuzwa na iweje lipate nguvu mwaka 1992?

Nimalize kwa kusema umasikini wa mtanzania na maendeleo duni ya nchi hii kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya kuwa na mfumo wa chama kimoja kwa miaka mingi siku za nyum
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad