Mwanariadha Oscar Pistorius amekutwa na hatia ya kuumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp ikiwa ni siku moja baada ya kutopatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.
Akisoma hukumu ya Oscar muda mfupi uliopita, Jaji Thokozile Masipa ameeleza kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa aliua kwa kukusudia.
Mahakama imemkuta na hatia pia katika kesi ya kutumia silaha vibaya.
Kutokana na kukutwa na hatia hiyo, Pistorius anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela.
Hata hivyo hukumu ya idadi ya miaka ya kifungo hicho inategemea sana maamuzi ya Jaji kutokana na sababu na utetezi wa mtuhumiwa.
Bado hakimu anaendelea kusoma hukumu ya Oscar Pistorius huku dunia ikishuhudia moja kwa moja kwenye runinga muenendo wa kesi hiyo.
Oscar Pistorius Akutwa na Hatia ya Kuua Bila Kukusudia
2
September 12, 2014
Tags
ANGEKUWA TANZANIA HUYO WALA ASINGEFUNGWA,LKN HUKO KWA WENZETU ATAFUNGWA TU,MAANA HUKU ALIYEMUUA KANUMBA BILA KUKUSUDIA,ANATANUA TU,MAANA ANAJUA HAWEZI KUFUNGWA,TANZANIA SIKU ZOTE JELA NI WATU WANYONGE,NA
ReplyDeleteISSUE YA KANUMBA TOFAUTI SANA NA HII. HUYU KAUWA KWA KUSUDIA KABISA. RISASI YA KWANZA TU ANASIKIA SAUTI YA MPENZI WAKE HALAFU ANAENDELEA KUSHUTI TU MPAKA NNE??? MIYE HAPO NDIO PANANISHANGAZA!!!
ReplyDelete