Sakata la Okwi Kuhusu Yanga na Simba, Hili Hapa Tamko la TFF

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba 7) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.
Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika Ukiwa ni mkataba wa pande mbili Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
Yanga ikiwa kama mwajiri haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe,Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru,hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo gabachori Yusufu Manji ni dhulumati mkubwa, alitaka kumdhulumu mtoto wa watu huku anajisifia eti ana hela ndefu kiasi cha kuweza kuinunua Simba yote, nyooooooo!!! Alitaka amchezeshe mpira bure, halafu anakimbilia TFF kumdai Dola 700,000, mwizi mkubwa we Manji na yanga yako!! OKWI SHIKAMOO......... Manji chaliiiiiiii!

    ReplyDelete
    Replies
    1. mona joto hasira na matusi tele..ukitoa mawazo yako ki ustarabu utamwagiwa tindikali....ovyooo.jifunze matumizi mazuri ya mtandao.

      Delete
    2. mbona joto hasira na matusi tele..ukitoa mawazo yako ki ustarabu utamwagiwa tindikali....ovyooo.jifunze matumizi mazuri ya mtandao.

      Delete
  2. Ila jamani Okwi kajua kucheza na akili za WaTanzania,
    ni OKWI kafanya hivi na vile,na bado nina uhakika atakinukisha tena,TUPO!

    ReplyDelete
  3. TFF yenyewe ni Usimba/Uyanga.
    TZ tutachezewa mpaka basi

    ReplyDelete
  4. sikio la kufa halisikii dawa,na huko simba atafanya madudu tu.tutaona

    ReplyDelete
  5. Sheria huwa zinapindwa,na hapa TFF WAMEPINDISHA sheria kwa maamuzi hayo,kiukweli Yanga hapa wakisimama na mwanasheria mzuri
    hii kesi wanashinda kabisa na tena watavuna hela nzuri sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mmmh sijui kama watashinda,maana usimba na uyanga
      utapelekwa mpaka huko unakodhani wakiendesha hii kesi yanga watashinda.

      Delete
  6. Yanga wasimwachie huyu choko apite hivi hivi, lakini kama hakula pesa zao basi watakuwa hawana jinsi, wamwachie tu, cc wanayanga hatumtaki huyu choko, bado hajajitambua!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad