Ajali hiyo imehusisha basi la MWANZA COACH T736 AWJ lililogongana na gari lingine la J4 Express T677 CYC. Miili ya marehemu na majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya mkoa iliyopo Musoma mjini.
Akizungumza na Bongo5 leo, Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba amesema uamuzi huo umeendana na majadiliano na wasanii jinsi ya kutoa msaada kwa wahanga.
“Tumefikia uamuzi wa kuahirisha tukio hili ambalo linahusu watanzania wengi, idadi ya watu 60 kwenda mbele, ni namba kubwa sana, hatuwezi kusema tuendelee na tamasha kwa leo. Kwahiyo pamoja na kwamba maandalizi yote yalikuwa tayari kabisa, watu walio =nunua tiketi zao tumekaa na uongozi pamoja wasanii wenyewe tumeona ni lazima tuwape heshima wale waliopoteza maisha yao, kuomboleza pamoja nao waliopotelewa na ndugu zao. Lakini pia tunawapa pole wale waliopatwa na majereha. Leo yenyewe sasa hivi wasanii, wanajitolea kila mtu anajitolea kiasi kidogo kununua mahitaji ya kupeleka hospitali. Kwahiyo hapa kuna kundi la wasanii ambalo wamekwenda kununua vifaa vya kuwasaidia wagonjwa na taratibu nyingine zinazoendelea,” amesema Ruge.
Baadhi ya wasanii walipata nafasi ya kuzungumza na Victoria FM na kutoa pole kwa wakazi wa Musoma pamoja na mkoa wa Mara kwa ajali iliyotokea.
Barnaba
Tumeguswa kama binadamu wenye kupenda wenzetu waendelee kuwepo, kwa sababu huwezi jua na wenzetu wana mchango gani kwenye hii sanaa tunayoifanya. Mungu hawalaze mahali pema peponi, tufanya maombolezo.
Christian Bella
Kwanza tunawapa pole wale wote ambao wamepata matatizo kwa siku ya leo, pia ninawapa pole wale wote waliokutwa na matatizo.
Edu Booy
Kitu ambacho ninaweza kusema mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, hii ni njia ya wote dunia ni daraja sote tunavuka.
Roma
Pole kwa watu wote waliofiwa na ndugu zao, tunajua tumepoteza mama zetu, baba zetu na ndugu zetu , sisi wasanii tumewapoteza mashabiki wetu na tunajua kabisa kuna watu walipanga kuhudhuria Serengeti fiesta ila leo hawapo tena. Kwahiyo ni jambo ambalo kweli limemgusa kila msanii na mdau ambaye alikuja kwenye Serengeti Fiesta. Tunawapa pole tena na tunawaombea wote waliotangulia mbele ya haki.
Shilole.
Kiukweli nimepoteza ile furaha yangu ambayo nilikuwa nayo kwa sababu ya kupata taarifa za msiba wa ajali ya gari kiukweli nikiwa kama mwanamke imeniuma sana ila siwezi kupishana na kazi ya mwenyezi Mungu.
Blog ya Jiachie imeeleza kisa cha ajali hiyo kuwa:
Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndoho kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa
Hizi ni baadhi ya picha katika eneo la tukio hilo.
Show ya Fiesta Musoma Yaahirishwa Kufuatia Ajali ya Mabasi 2 iliyosababisha Vifo vya Zaidi ya Watu 45
2
September 05, 2014
Tags
Innalillah waina illah rajiun
ReplyDeleteTunawaombea waliopoteza maisha Mungu awape pumziko la milele Ameen na majeruhi Mungu awape nguvu na uzima hii ajali mbaya sana eee Mola tuepushe na haya Ameen!!!
ReplyDelete