'Si Lazima Kujua Kingereza Kwani Mie Muingereza, Hata Messi Hajui' - Ray

Mkurugenzi wa Kampuni ya filamu Rj Company,Vicenti Kigosi amesema si lazima kujua Kingereza maana hata Messi hajui, Ray amesema hayo alipokuwa akichat Live na mashabiki zake kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live

kinachokukutanisha na watu mahiri kila siku ya jumatano kuanzia saa sita za mchana mpaka nane kamili.
SI LAZIMA NIJUE KIINGEREZA
Mkali huyo ambae kwa sasa anachukuliwa kama moja ya watu wenye mafanikio katika tasnia ya filamu nchini ambae pia ameshawishi vijana kibao kuingia katika tasnia hiyo amefunguka na kuweka wazi kuwa suala la lugha ya kiingereza kwake ni changamoto lakini si jambo la ajabu sabgabu kuna watu wengi maarufu duniani wanapigwa chenga na lugha ya kiingereza.
Prince Dully >>>>Mbona haujui kingereza au uliishia darasa la saba,nini?
RAY Kigosi >>>>>>Hata messi hajui kiingereza kwani mimi muingereza nijue Kiingereza.
CHUCHU MCHUMBA WANGU
Msanii Vicent Kigosi ambae katika hizi siku za karibuni ilisikika kuwa yupo katika mahusiano na msanii mwingine wa filamu ambae anafahamika kama Chuchu Hansi hivyo ilipelekea mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV kutaka kujua ukweli juu ya mahusiano hayo na kama kweli jamaa anampango wa kumuoa binti huyo au laah,na majibu ya Ray uyalikuwa kwamba wawe watulivu muda utakapofika ndio watajua ukweli wote juu ya suala hilo.

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jifunze english ww acha uzamani huo. messi ni tajiri na ww je?

    ReplyDelete
  2. hehehe kiitu yai limekataa mchezo!!utakaakucheza michezo ya kiswahili mpaka unazeeka!!wenzio wanataka watoboe hollywood!!wewe hata nollywood hutaweza kwisha habari!!

    ReplyDelete
  3. Wewe kauzu ray ,tutolee mfano wa mwafrica alietoboa Hollywood bila kujua kiingereza mwezio messi yupo spain na anaongea spanish ndo lugha yake ya taifa, na ata akienda italy atajifunza kiitalia, sasa wewe subiri hapo hapo sinza mori.

    ReplyDelete
  4. Acheni ukiritimba, Kiingereza ni ruga tu za hapa Duniani ambayo unaweza kutaka kuijua au usitake, ni uamuzi tu, kama ukiona Dili zako zitakuwa kwa nchi znazo zungumza Kiingereza jifunze, kama unapiga dili zako kwa Nchi zinazo zungumza Kifaransa kifunze, kichina jifunze, hizo ni ruga tu za kujifunza miezi fulani sio miaka akiamua na akiona ataanza kuvuka mipaka ya Nchi zinazo tumia ruga nilizo zitaja hapo juu atajifunza.

    ReplyDelete
  5. Tatizo Watanzania wajua kiingereza ndio kila kitu, nenda china na kiingereza chako kama hujatafutiwa mkarimani mtaani, Elimikeni kidogo,

    ReplyDelete
  6. kweli kabisa nenda china na english yako huone cha moto. au nenda urusi pia kama kuna kiingereza kule !!! kiswahili bana bonge la lugha najivunia kwa saana ... au nenda japan kama kuna kiingeeza kulee!!

    ReplyDelete
  7. Kila mtanzania mwenye kipato kama cha Ray ana uwezo wa kujifunza kingereza au lugha yoyote kimataifa na sio lazima mpaka vyuoni tu,huko mitaani kwetu
    walimu wa kiingereza wamejaa tele kila kona,Ray hapendi tu kujifunza na ni kama karidhika vile na kufanya kazi hapa kwetu tu,haangalii mbele,yupoyupo tu.

    ReplyDelete
  8. Sio kiingereza tu inabidi aende Shule akafute huo ujinga aliokuwa nao hovyoooooooo..........Ndio tatizo la watanzania hamuangaii wala kukubali kuwa mataifa mengine yanatupiga bao kwa sababu ya hiyo lugha.

    ReplyDelete
  9. Anony 10:02AM SAFI SANA!! umempa ukweli wake bila kupepesa ni straight hit Ajifunze na Aangalie mbalii.

    ReplyDelete
  10. Mmmh,nyie mnaosema kingereza sio dili hamjielewi.
    Mimi nimemaliza kidato cha nne tu sina uwezo wa kuendelea na masomo mengine ila najifunza kingereza kwa kuwa sitozwi hela nyingi.Hivi Diamond asingejua kuongea kingereza angefika hapo alipo?angeongeaje?si angeibiwa sana kama angetegemea kila kilichoandikwa kwa kizungu asaidiwe na mwenye kujua kizungu?Nimepata kazi ya kulea watoto kwa balozi fulani, watoto hawajui kiswahili, lugha wanayojua ni kingereza na kifaransa tu,haaaaaaaaa patamu hapo!mbona imebidi nijifunze kizungu maana kazi napenda,wananijali,na wana mpango wa kuondoka nami muda wao wa kukaa bongo ukiisha.KINGEREZA NI DILI JAMANI. Wee Ray soma kingereza kaka.

    ReplyDelete
  11. Hata mimi nataka kujua kizungu kwa bidii zote,watoto wa dadangu wakitoka shule wananipa changamoto kwelikweli,ni yes, no ,yes, no kwenda mbele,na nitakijua tu uzuri sioni aibu kuongea,wakinikosoa nami nimo tu narekebisha nilipokoroga siku zinaenda.ray soma kizungu kakangu,kwani hukumbuki Marehemu Kanumba (R.I.P).

    ReplyDelete
  12. Achezi hizo tukipendeni kiswahili ray big hup jifunie lugha yako ukipenda kujifunza english nenda lkn sio km hao watumwa bila english hkn maisha washambaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad