Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,Samweli Sitta,bila haya wala kumungunya maneno,amethubutu kusema baadhi nyaraka zinazosomwa makanisani ni upuuzi kabisa.
Akiwakaribisha wageni ambao ni waumini wa makanisa bwana(sidhani kama anafaa kuitwa mheshimiwa) Sitta amesema na hapa namnukuu "muwe waangalifu huko makanisani kwani baadhi nyaraka zinazosomwa huko ni za kipuuzi".Huenda sijanukuu maneno yote kwa usahihi ila kikubwa amesema nyaraka hizo ni za kipuuzi!
Wadau,nafikiri wote mnankumbuka waraka wa jumuiya ya kikiristo Tanzania(CCT) uliokuwa unasomwa makanisani na waraka huo ulikuwa unapinga kuendelea kwa bunge hilo.
Sasa mdau tafakari mwenyewe mzee Sitta alikuwa anaongelea nyaraka gani na utapata jibu alafu jiulize mwenyewe athari ya kaulu kama hiyo kwa mchakato huu na Taifa kwa ujumla.
Alafu,hivi kila mwenye kuvaa suti na kuwa na mnvi anastahili kuwa kiongozi?
angalia sana sitta ulafi wa pesa na madaraka utayoyataka utakupeleka pabaya
ReplyDelete