Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kuwakumbusha wananchi kutumia njia ya mawasiliano ipasavyo ili kujijengea heshima kwani kwa sasa hatua kali za kisheria zimeanza kuchukuliwa kwa wale wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Times fm, Meneja mawasiliano wa (TCRA) Inocent Mungy amesema kuwa ipo haja kwa wasichana kujiheshimu kwani picha nyingi mbaya zinazoonekana kwenye mitandao hiyo ni zao.
Naye Mkuu wa kitengo cha masuala ya watumiaji wa mitandao Isack Mruma amesema watu wanapaswa kuelewa matumizi sahihi ya mitandao na lazima kuwe na usiri wa akaunti za mitandao ili kuweza kuepukana na matatizo ya usambazaji wa picha mbaya kwenye mitandao hiyo.