Ukichukua Fedha Benki Bila Ulinzi Sasa ni Roho Mkononi

Ni roho mkononi. Hayo ndiyo maneno matatu yanayofaa kuelezea hali ilivyo jijini Dar es Salaam na maeneo kadhaa nchini kwa sasa, hasa pale mtu anapobeba fedha nyingi.

Matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha yamekuwa sugu na kusababisha wananchi wanaopeleka au kutoa fedha benki kuvamiwa, kujeruhiwa au kuuawa mchana kweupe na majambazi wanaotumia pikipiki.

Wananchi wamekuwa wakihoji ni kwa jinsi gani majambazi hao hupata taarifa za mtu aliyekwenda benki ama kuweka au kuchukua fedha.

Mkazi wa Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Salum Mashati alisema: “Haiingii akilini, utasikia mtu kaporwa fedha akitoka benki. Eti majambazi wanasema kabisa toa hizo milioni 20, wanajuaje kuwa una kiwango hicho? Huenda watu wa benki wanashiriki uhalifu huu.”

Hata hivyo, meneja wa tawi moja la benki lililopo Mlimani City, ambaye hakupenda jina lake litajwe alikanusha madai hayo... “Si kweli kwamba benki zinashirikiana na majambazi kufanya uhalifu huu. Kwanza wahudumu (bank tellers) hawaruhusiwi kuingia na simu wanapohudumia wateja.

Nini Kifanyike?
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. .mwongo we meneja, ma-teller mara nyingi wanatumia simu zao za mkononi wakiwa kazini... acha kusema uongo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad