Ukweli kuhusu Maisha ya Watanzania Walioko Ughaibuni



Naona kumekua na maneno meengi kuhusu watanzania waishio ughaibuni.
Mimi nimeishi Scandnavia kwa muda mrefu ila baada ya kutimiza malengo yangu nilirudi nyumbani for good.Kwa sasa huwa ninakwenda mara kwa mara kwa sababu ya kibiashara kisha ninarudi nyumbani.

Kusema ule ukweli wa Mungu,kwa watoto wa maskini kama mimi ulaya ni bora kuliko bongo.Hapa nitaiongelea ulaya kama ninavyoifahamu mimi.Mimi mzee wangu hakua tajiri kama mzee wa Le mutuz,Tanzania niliyozaliwa mimi na kukulia ni tofauti sana na Tanzania aliyozaliwa na kukulia kaka yangu Le Mutuz.Mim Mungu alinijalia sana akili za darasani lakini kutokana na umaskini wa wazee nilishindwa kuendelea na chuo.

Ikatokea zali nikaenda scandinavia,nilienda kule nikiwa na malengo mawili,kusoma na kutafuta mtaji wa maana wa kijiajiri.Mungu alinisaidia,nimesoma,nina masters yangu,nina nyumba sita nimepangisha,nyumba moja ninafanyia biashara zangu na moja ninaishi na wadogo zangu na moja iko mkoani wazee wamejisitiri.Nina viwanja na mashamba.Vyote hivi nisingekuwa navyo leo kama nisingeenda ughaibuni.

Pia Mungu alinisaidia nikakusanya pesa ambazo nilitumia kujiajiri.

Mimi niliajiriwa kwenye kampuni ya kutengeneza magari.Huko nilikua na waafrika wengine wengi tu.

Sio kweli kwamba sehemu pekee wabongo waliyo nayo ni kwenye birthday za sebuleni tu LOL.Ulaya kuna viwanja vya maana bana za kula bata bongo itasubiri sana tu.Kitu kinachofanya wabongo wakusanyike kwenye hivyo vipati hadi nadhani ni ile hali ya kufurahia kukutana na wabongo wengine.Pia sio kila mtu anapenda kuwa kwenye hiyo mikusanyiko ya wabongo,mimi ni mmoja wa watu ambao nilikua sipendi kujimix na wabongo wenzangu.

Suala la kwamba wabongo walioko ughaibuni wana maisha magumu sikubaliani nalo.Kwanza kabisa idadi ya watanzania walioko tanzania wenye access ya internet inayowawezesha kusema wabongo wa ughaibuni wanateseka ni ndogo sana ukilinganisha na watanzania walioko bongo wasiojua hata internet ni nini.

Mimi kwa sasa ninaishi Tanzania na ninafurahia maisha ya hapa sababu ughaibuni imenisaidia leo hii sihitaji kwenda kujambiana kwenye madaladala,leo hii nikipata ugonjwa usio na tiba ya kueleweka bongo naenda zangu kutibiwa Scandinavia,mm nina uraia wa scandinavia tayari.

Hakuna binadamu yeyote awe muafrika au mzungu au muarabu hata awe amechoka vipi financialy aliyeko scandinavia anayelala njaa eti kisa hana hela ya chakula.Kwa Tanzania kila jua linapokuchwa kuna mamilioni ya watoto na watu wazima wanalala njaa.

Scndinavia inaongoza kwa uchache wa vifo vya watoto na wazazi,kwa Tanzania hebu tuchukue sekunde tano kuwaombea R.I.P dada na mama zetu watakaokufa wakati wakijifungua usiku wa leo.Tanzania mama zetu wanajifungua huku wakitzabwa makofi na manesi.Dada zetu waliko ughaibuni wanajifungualia katika mazingira kama mtu yuko hotelini,hata wanaojifungulia Aghakhan watasubiri sana compare na wanaojifungulia hospitali za serikalini ughaibuni.

Tokea nimeishi ughaibuni sijawahi shuhudia umeme ukikatika wala maji.Huwa wanayafunga tu kwa masaa au kuukata umeme kwa masaa na hapo mnapewa taarifa kuwa saa fulani mpaka saa fulani maji au umeme utazimwa.Sijawahi kuona watoto wanaotembea peku na kaptura zimechanika kwenye masaburi.Sijawahi ona mtoto akishindwa kusoma kwa sababu mzazi hana pesa,sijawahi ona mtu anakufa kwa kukosa elfu mbili ya kununua dawa,sijawahi ona watoto wenye utapiamlo,sijawahi ona watu wakitembea pekupeku,sijawahi ona ambulance za vibajaji LOL,sijawahi ona wakulima masikini kama hawa wa Tanzania.

Scandinavia maji huchemshi,unafungua bombani unakunywa,ukitaka ya baridi au ya moto kila wakati yapo.

Wkati naishi ughaibuni nilikua sina gari binafsi,japo magari ni bei chee sana kila mtu anaweza kuwa nalo cha muhimu tu uwe na vibali vya kukuwezesha kupata driving licence.Sikuhitaji gari binafsi kwa sababu usafiri wa public ni wa starehe.Baada ya kurudi bongo imenibidi tu niwe na usafiri sababu daladala kusema ukweli ni hiyo shida tu lakini ni mateso.

Wabongo walioko ughaibuni wanabezwa kwa kazi wanazofanywa,fine,hata mimi huko kwenye kampuni ya magari sikuwa nafanya kazi niliyosomea,ila ukweli ni kwamba nilikuwa nalipwa vizuri,wakati naanza nilikua nalipwa kama milioni sita za madafu kwa mwezi.Baadae waliniongeza,sasa kwa mtoto wa maskini kama mimi ukiniambia nilivokua ughaibuni nilikua nateseka nakuona unaongea kichini maana mdingi wangu angekua nazo hizo nisingeshindwa kwenda chuo bongo wakati kichwani kuko vizuri.

Hata wanaosafisha wazee hakuna anayepokea chini ya milioni nne za madafu kwa mwezi.Hapo nimetaja kima cha chini.

Kitu ambacho ambacho kwangu kilikua kinanipa stress enzi naishi ughaibuni ni kwamba sijawahi kufeel at home.Hii hali ndiyo ilinifanya kusave na kufanya kazi kwa bidii hadi nikatimiza malengo yangu nikarudi home.Kwa kifupi social life ya ughaibuni sucks(,huu ni mtizamo wangu).

Inshort kwa upande wangu mimi hata wale watanzania wanaoishi ughaibuni bila vibali mateso yao hayafikii hata theluthi ya mateso ya watanzania masikini walioko Tanzania.

Ughaibuni ni kweli kuna maisha ya ghali,ila ukiishi kwa malengo yako hakuna asiyefanikiwa.Pia ukiamua kuwa mtu wa bata ughaibuni utakula bata za maana kuliko wala bata wa bongo.

Ni kweli wahamiaji wengi(sio wabongo tu) wanafanya kazi za wazee,kusafisha na nyingine kama hizo ila ni ukweli pia kuwa wapo wapo wengi tu wenye kazi zao za maana.
Pia wewe secretary au mfanyakazi kwenye kampuni ya simu bongo na nyingine kama hizo hebu jiulize unapata shilingi ngapi kwa mwezi hadi umcheke mwenzio anayesafisha wazee na kupata milioni zake nne kwa mwezi?

Kitu ambacho wabongo wamewazidi walioko ughaibuni ni good social life tu.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Daaah umeongea point and that's so true. Mi sina comment kabisaaa

    ReplyDelete
  2. Mi natunza wazee,mbali na matumizi mengine nimesave $20,000.(Hapo nimesema mbali na matumizi mengine)na sina anayenitegemea Bongo.

    ReplyDelete
  3. Yaani umeongea vizuri sana. Ni kweli maisha ya watanzania wanaoishi ulaya ni bora sana. Kwa kuongeze unapozaa mtoto ,mtoto anakuwa anapewa pesa kila mwezi na serikali mpaka anapotimiza miaka 18.

    ReplyDelete
  4. Daa. Nitafutieni mchongo huo nami hata wa kulea wazee. Kwani maisha ya bongo ni shidaaaaaaaaaa tuuuuuuuuuuu. Ila siyo ya kujiuza mwili tu.

    ReplyDelete
  5. Mimi nami naishi huko huko, ni tofauti sna na maisha ya hapa kwetu bongo, nilifanya kazi kwa mwaka nikaingiza hela nzuri, baada ya hapo kazi ikaishia, sasa kwa kuwa nilingiza hela nzuri na nimeripa kodi, nitaendelea tena kulipwa kwa miaka 2. Kutokana na balance niliyolipa kodi na hela niliyoingiza, ukiesabia kwa madafu kama mil. 3 ya kibongo hiyo nalipwa tu bila hata ya kazi, endapo tu kama sitakuwa na kazi kwa muda wa miaka 2. hiyo nnalipwa upate hela ya kujikimu, wakati unatafuta kazi nyingine,ndani ya hiyo miaka,

    ReplyDelete
  6. well!! umemaliza kila kitu umeelezea vizuri sana, maana watu hawaishi kuwananga walioko ughaibuni kwamba warudi nyumbani, kwani ughaibuni wanateseka kwa ukweli hata kama ughaibuni ni kubaya vipi haitakaa kamwe ikafikia maisha ya african hata kwa dawa ughaibuni ni ughaibuni tu.Hatamponde vipi ulaya itabaki kuwa ulaya america itabaki kuwa america huwezi hata siku moja kufananisha kifo na usingizi ulaya kuna utu huna wasiwasi wa kuvamiwa na majambazi, hakuna foleni za kijinga,hakuna rushwa,usawa kwa wote haijalishi wewe ni masikini au tajiri, haki sawa umema wa uwakika, maji enternet unapata bila shida yaani ni raha kwa kwenda mbele sema tu una miss home kwa sababu ulishazoea kukaa na ndugu, marafiki ,majirani n.k na hatashida zao pia kwa hiyo watu wasiponde kwa sababu tu wao wameshindwa kupata bahati ya kuja ulaya maana naye kupata bahati yaku sio mchezo ni bahati ya pekee sana

    ReplyDelete
  7. Dah mi mwenzenu maisha yangu yanafanana kiasi fulani na msimulizi hivyo kama vp kama kuna mtu ana access ya ughaibuni anitafute i'll pay for that i promise.....@+255683 683 750

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad