Nimekuwa nikiona wapinzani wa Lowassa ndani ya ccm wakihangaika kila njia wakijaribu kuangalia ni namna gani wanaweza kumshughulikia jembe hili la kaskazini linalo mtanguliza Mungu mbele wakati wote wa mambo yake.
Lakini leo nimeona walau niwape ushauri kidogo baada ya kuona kila mnapo jaribu mnaangukia pua ni kwamba Lowassa ni mtu anaye mcha Mungu tofauti na wapinzani wake ndani ya CCM wamekuwa mara nyingi wanatumia nguvu za kiza na fedha nyingi wakifiri watamuweza Lowassa, lakini cha kushangaza mzee Lowasa amekuwa akizidi kuchanja mbuga kila kukicha na nyota yake kuonekana iking'ara kila siku japo kafungukiwa.
Naomba niwadokezee siri kuwa mgeukieni Mungu achaneni na nguvu za giza na mazingaombwe ndio njia tu ya kuweza kupambana na Lowassa japo mpaka muda kama ni soka basi tunaweza kusema Lowasa anaongoza kwa bao 3 bila,
Mkizingatia ushauri wangu mtasonga mbele epukeni kwenda kuchanjwa chale mwili mzima mrudieni Muumba atawasaidia.
By kiloriti
Wewe nani wa kujua ni mcha Mungu, kutoa pesa chafu anazotoa kanisani, kwenye misikiti, na kwenda kusali kanisani unafikiri ndiyo kigezo cha ucha Mungu, ya Mungu mwachie Mungu. Sisi tumtizame yeye na amedhihirisha hafai kuwa Raisi kwa yale aliyofanya akiwa Waziri Mkuu hadi kufikia akastaafu.
ReplyDeleteuna uhakuka alifanya kwa kupenda akiwa waziri mkuu au alishikishwa?
DeleteLowasa Uraisi wa Tanzania utakuwa ni ndoto kwake, kama anataka kuendeleza siasa abakie huko huko wilayani na Ubunge wake au miaka 5 ijayo atasahaulika kabisa!
ReplyDeleteKama yeye ni mtu safi basi hadi leo tungetambua mchango wake kama waziri Mkuu lakini kashidwa kuwajibika na kashifa tele za ufisadi wa hali ya juu.
Mfano wa kuigwa ni Mizegwe Pinda na jembe la maana maana kazi zake tunazikubali kaamuwa kuweka wazi utajiri wake na hana ufisadi wa aina yoyote ni mtoto wa mkuliima nakubali na hili.
Japokuwa alitubeza waZanzibari kwa kauli yake ya kuwa Zanzibat si nchi lkn mazuri yake yanafuta yoote aliyoyatamka na ni matumaini yangu akiwa madarakani Zanzibar itapata uhuru wake kamili.
wee pupet tu
DeleteAliyenzisha mjadala huu ni mnafiki, kumuta Lowassa jembe la Kasikazini ni sera siri za Chama chenu cha Wakasikazini na sio za chama chake cha CCM, Lowassa ni wakitaifa; CCM wakimtenga tu wamekwisha kisiasa. Msidanganywe ndani ya siasa hutazamwa nyota ya mtu kama walivyofanya Afrika ya Kusini mbali ya kashifa nyingi za Zuma, Lowassa nyota yake kwa Watanzania tuliowengi iko juu, CCM ikimtenga tu na sisi wengi tunaitenga kwa kutupendekezea mgombea tusiomtaka.
ReplyDeletehayo yote aliyoyafanya huko nyuma, ufisadi, na urafi wa ufujaji wa mali za umma, amesha litambua kosa lake, na ameshajua nchi wapi wanaipeleka pabaya, kwa hiyo kesha jifunza mengi tu, mabaya na mazuri, anaonekana ni jembe, Lowassa
ReplyDeletesasa huyu ndio atakae komesha urafi, na ufujaji wa mali za umma, kama ufisadi, na nchi kitaeleweka, kama Elimu nzuri, mishahara mizuri kwa walimu, mahospitali mazuri na madawa ya kutosha, pamoja na miundo mbinu, hiyo ndio kazi ya nchi, na kuangalia wananchi wake. anaonekana anaweza, huko kwengine ni bla bla, mambo yatakuwa yale yaleee.
ReplyDeletebora Alshabab wachukue nchi ieleweke moja kuwa roho zetu zimewekwa rehani, cheki walivyojijengea majumba ya kifahari ufukweni, idadi ya viwanja anavyomiliki ndio usiseme, wewe hata chumba kimoja huna, huyu mtu hafai jamani anarumia kivuli cha Mungu kutufumba macho watanzania Hana jipya Lowasa, kwani lazima awe Rais? kwanini asibaki kuwa mwanachama tu na aendelee na hizo harambee zake? tuamke jamani return ya hiyo misaada ni kubwa sana endapo atapata huo Urais, bora hata mtoto wa mkulima awe Rais maana tunajua tukikosea tu ni kupigwa inafahamika
ReplyDeleteAnaeitwa mchawi, Mpe huyo mchawi mtoto wako akulelee, atamwangalia kwa jicho la tatu kumfutia hizo tuhuma anazopewa na wabaya wake. Huyu mchawi ni Lowassa kipenzi cha wengi aliyepolwa uwaziri mkuu kwa tuhuma za wabaya wake ili aukose urais 2015, wananchi tumegundua fitina dhidi ya Lowassa, jembe la wengi, mtoto ni serikali 2015 huyo mtoto apewe mchawi Lowassa amulee, akipewa mwingine atamloga.
ReplyDeleteumeonaee mchawi mpe mwana, wamemchafua na skendo zao but ukweli unajulikana wanakaa uso zinawashuka huyo ndio dawa ya wezi ccm ndio maana hawamataki maana wanajua akiingia madarakani wote jela
ReplyDeletemtasema yoooote lkn Lowasa akipata nafasi atakuwa tu urais. Sisi wenye akili tunatambua ila mambulula mtahangaika saaasna!
ReplyDeleteKm kuna kosa kubwa ambalo mtakuja jutia ni kumpa nchi hyu baba,najua weng mnamsapot ni kutoka kanda ya kwao,tuachane na ukanda jmn angalien maslah ya watz wenzenu,MTU anatumia mamilion tote hyo tena ya kwake ili aingie ikulu,hamuon kuwa ni ttzo kubwa hlo
ReplyDeletetoa sababu ni kwa nini asipewe.... achana na personal feelings
DeleteSasa hayo mamilione atajua kwa kuyarudishia wapi, hayo hayo, mamilioni atajenga mahospita mazuri au atarekebisha, na madawa yatakuwa ya kutosha mahosptalini, na mashure mazuri na barabara za kueleweka, na ufisadi utakomeshwa, kwa kuwa yeye alishaupitia huo ufisadi, na ameona mazuri yake na mabaya, sasa ufidi i weee no, twa taka kwenda mbele, wengine hao wataendelea kulindana na ufisadi utakuwa pale pale, mambo yale yale. huyu atalekebisha tu nchi haifai, inanuka kila nyanja, huko kwenye hopital kubwa, ya rufaa kote ziiii, madawa hamna, shule tabu, za kayumba, kila kitu ivyo ovyo sababu ya ufisadi umezidi, unaua Taifa, kwa maslahi ya watu wachache, wezi wa hili Taifa, tuamke wanachi
ReplyDeletehapana Lowasa hafai, anajitahidi tu kutafuta huruma kwa watanzania, halafu tukikaa vibaya hawa watu wa kanda yake nao watatupeleka pabaya, tutumie akili na sio ukabila au tunakotoka, kama hajaiba yeye na wezi alikua anawajua, kwanini asiwataje? ninachojua mimi ni kuwa ukweli unamuweka mtu huru na kumtetea popote pale, sasa huyu anaekuwadia kuwa Rais hafai sababu ni muongo si mkweli, Rais ukishakua hueleweki na maelezo yako mpindisho wananchi tutafika wapi, aseme mabilioni ya Richmond yako wapi, na hizo pesa anazotoa misaada usiku na mchana kufuata madaraka anatoa wapi, mmh huu uchu wa madaraka utatupeleka pabaya hana utu kabisa hatufai huyu, bora hata Mkapa arudie urais na si huyu Lowasa, hakuna aliemtoa uwaziri bali ubadhilifu wake na ufisadi uliotukuka ndio ulimfanya ajiuzulu, asitafute mchawi, kwakua yeye anamuomba Mungu na kumtegemea, hata sisi tunamuomba Mungu vilevile atuepushe na kiongozi fake, ukweli utafahamika
ReplyDeleteKwanza Hilo hafai kuwa rais wala nini uwaziri mkuu ulimshinda sasa mnataka kuwa rais... Ni sawa na house girl asiyajua majukumu yake unaamua kumfanya maza house fyuuuu na upofu wake WA macho.. Kwa now days Ni spans mkononi
ReplyDeleteJamani mbona watu wengi tumeshaona Rais ajae atatoka ZANZIBAR?
ReplyDeleteZungumzia ni kiongozi yupi anafaa kuwa Rais kutokea Zanzibar,sio Bara.
Mmesikiaaaaaaaaa!
raisi ajaye ni jembe lowasa mtu mwenye uwezo wa kuchukua maamuzi magumu,anatufaa
ReplyDeleteLowasa ndo mpango mzima kwanza ni kiongozi mtendaji anajiamini,anao uwezo wa kuthubutu,muonekano una lipa kifupi appearance yake inasuit kweny upresident. Sio huyo Pinda lisura baya km nini hata huko nje akienda kufanya ziara ulimwengu utatucheka km c kutushangaa
ReplyDelete