Wanaume Wanaowatelekeza Watoto Wao Nchini Kenya Wanakiona Cha Moto Kupitia Facebook

Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.

Kikundi cha wanaume watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya.

Mtandao huo tayari umepata mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri, Huu Ndio mtandao ulio Weka Wazi Kuwa Prezzo hatoi matunzo kwa Mtoto wake hivi karibuni

Kwa nini mwanamume mwenye uwezo amtyelekeze mtoto wake? Baadhi ya wanaume wanalalamika kuwa wanawake ni wajanja kwani wanashika mimba kwa njia za kijanja.

Na je Jackson Njeru mwanamume aliyeanzisha ukurasa huu wa Facebook hahofii maisha yake? Hilo ni moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi wa BBC Dayo Yusuf

Sikiliza Hapa:

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii mimi nimeipenda sana, pia nawapongeza kwa kuitumia mitandao kwa kuelimisha jamiii nasio matusi na mambo yasiyoeleweka ,hongera mdau uliyeanzisha hiki kitu lazima mwanaume uwajibike sio ujue kupachika mimba hlf hujui kuitunza tena wakomeshwe kabisa na huku TZ pia watu waige mfano huo mana machokoraa wapo wengi pasipo na sababu hivi vituo zitapungua jmn mana siku hizi vipo vingi chanzo ni nyie wababa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad