MBRAZIL Marcio Maximo amepoteza mechi yake ya kwanza akiiongoza Yanga baada ya kukubali kipigo ‘swaafi’ kabisa cha mabao 2-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar, uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro jioni hii.
Katika mechi hiyo ya kukata na shoka, Mbrazil mwingine, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ naye ameweka rekodi ya kukosa mkwaju wa kwanza wa penalti akiichezea Yanga katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu.
poleni wana Yanga wenzangu!! inauma sana lakini salama!!
ReplyDeleteMimi sio Yanga wala Mtibwa,ila nathubutu kusema Yanga wamenyongwa sana,
ReplyDeletekwenye ule mchezo refa aliwabeba sana mtibwa.Pamoja na kwamba nilitaka Yanga ifungwe
lakini sio kwa kuwaonea vile,kwa namna hiyo sijui kama soka letu litakuwa.Poleni sana Yanga.
Hata mimi nakuunga mkono mdau hapo juu,TFF wajaribu kufatilia msimu huu.
ReplyDeleteTusiwe mashabiki wa kufurahia timu yako ikishinda hata kama ilicheza vibaya.
TFF ya sasa ndio itatupelekea mpaka kuwa wa 160
ReplyDeletekwenye wiwango vya FIFA,tusubiri tu.Jirani zetu wanazidi kutuacha kisoka.
MNYONYE MNYONGENI,LAKINI HAKI YAKE APEWE.
ReplyDeleteYANGA WALIONYESHA SOKA YA HALI YA JUU HASA KIPINDI CHA PILI
ILA SIJUI HAWAKUMUWEKA VIZURI REFA?( KUMHONGA REFA )
Ndio mpira wa bongo,lazima yanga wakubali matokeo.
ReplyDelete