Zanzibar Yajitoa Rasmi Bunge la Katiba

Kukosekana kwa Waziri na pia mwanasheria Mkuu kujiondoa wote wakiwa wanaiwakilisha Zanzibar ,wajumbe walio wengi wameichukulia hali hiyo kama kujitoa kwa Zanzibar katika kutunga Katiba mpya kwani itakosa nguzo muhimu zinazohitajika kutoka pande mbili za nchi washirika wa Muungano.

Sababu zinadaiwa kujitoa kwa viongozi hao wakuu ni kutokana na mwenendo mzima wa kutunga Katiba ambao umekumbatiwa na Chama tawala kwa maslahi yao binafsi na kuondoa ile hali ya kuifanya Katiba hiyo iwe inatokana na maoni ya Wananchi kama yalivyowasilishwa kwenye rasimu ya Jaji warioba na tume yake ambayo imesainiwa na raisi wa Jamhuri wa Muungano. CCM hawakujali saini ya Raisi wala ghali wameutupilia mbali na kuchomeka waliyokuja nayo kwenye viroba.

wakuu hao kwa kuthamini taaluma yao ya uwana sheria hawakuwa tayari kushiriki kusaidia hila za CCM kugeuza na kupindisha maoni ya wananchi taaluma yao haiwaruhusu na hivyo wamejiengua kulinda heshima yao na vilevile kutokubali kuiwakilisha Zanzibar katika uchakachuaji wa Rasimu ya Jaji Warioba na tume yake ambayo imesainiwa na Raisi.

Inasemekana pia wakuu hao kabla ya kujiengua walimueleza Raisi wa Nchi yao kile kinachoendelezwa na kufanywa na CCM ndani ya bunge hilo la katiba na kuwa wao hawapo tayari kuendelea kukaa na kuandika jambo ambalo lilimpelekea Raisi wa nchi yao Nheshimiwa Sheini wafanye vile wanavyoona wao ndivyo ili kulinda maslahi ya Zanzibar na watu wake.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi kabisa tumechoka kunyanyaswa

    ReplyDelete
  2. Ccm inajifanya km miungu watu just to do what ever they want

    ReplyDelete
  3. We need our zanzibar back,CCM wanajifanya wao waungu watu kama kila wanachokitaka wao ndo kiwe na wasichokitaka wao kisiwe...Huu ulimwengu mwengine msituzinguwe,mshaongoza nusu karne hamna lililokuwa zaidi ya ongezeko la ugumu wa maisha....we need our zanzibar back...That's it...Hatutaki kulazimishwa kugandana na MUUNGANO wkt RAIS KARUME alishatwambia MUUNGANO ni kama kote,likikubana livuwe,mnatubana wenzetu tunataka kujivua msitulazimishe....tuacheni tupumue...

    ReplyDelete
  4. Tuuweni muungano hatuutaki

    ReplyDelete
  5. huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM, sio Zanzibar tu, lakini Tanzania kwa ujumla

    ReplyDelete
  6. Mnabana pua " tunata Zanzibar yetu" chukueni kwani huo muungano ulivivuta hivyo visiwa na kuviunganisha na pwani ya Tanzania Bara, mmetuchoka ondokeni. Mnasahau wosia wa MWL. NYERERE JUU YA DHAMBI YA UBAGUZI SASA MNAJIFANYA SUDAN YA KUSINI, kwaherini mkamalizane wenyewe kwa wenyewe mutuachie TANZANIA MPYA YENYE SERIKALI MOJA isiyo na Tanganyika wala serikali mbili.ndani yake. Watanzania bara mpeini Mzanzibari wembe wake mnang'ang'ania wa nini au mnataka tuvutane utukate na sisi ???????!!!!!!!!!!!!WAPENI TUMECHOKA.

    ReplyDelete
  7. Kabisaaa wazanzibari wabinafsisana,wanajiona kama miunguwatu.nakwanza mjitahidi wajukuu zenu wasome wasijekuwa naakili mbovu kamazenu.hatamungu alisema mshike sana elimu nyie shule hamna kelele Fujo na ubishi.wapeni kisiwa Chao wasituchoshe.mijitu gani inakurupuka tu.nanyie ccm acheni kujilimbikizia mali mmezidi ubinafsi kwani nyie ndio mle tu pekeyenu gaweni nchi yetusote hii.ubinafsi wenu ndo unaleta chuki

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad