Baada ya Kuachika Rose Ndauka Aangusha Sherehe ya Nguvu

SIKU chache baada muigizaji nyota wa filamu nchini, Rose Ndauka kutemana na bwana wake, Malik Bandawe, Jumanne iliyopita aliangusha bonge la sherehe iliyofana ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao, Ijumaa lilikuwepo.

Sherehe hiyo ya Rose, ambaye alizaliwa siku moja na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ilishuhudia mastaa wengi wa kike walioalikwa, licha ya kunywa na kula kwa kadiri walivyojisikia, lakini pia wakiwa wamevalia vivazi vilivyoonyesha sehemu kubwa ya miili yao.

Katika pati hiyo kulikuwa na vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi, huku pia vyakula vya aina mbalimbali vikipatikana, kiasi kwamba hadi gazeti hili linaondoka, pombe na vyakula bado vilikuwepo.
Lakini kivutio zaidi kwenye shughuli hiyo iliyoshuhudia pia Mussa Issa ‘Cloud’ anayekaimu uongozi wa Bongo Movie Unity akiutangaza upya umoja wao, alikuwa ni shoga mkubwa wa Rose, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’ambaye alionekana ‘akimkogesha’ fedha rafikiye wakati wa kutoa zawadi ulipowadia.
Akiwa kwenye sherehe hiyo, Rose alionekana kuwa mwenye furaha tofauti na siku chache zilizopita baada ya kukosana na mchumba wake huyo. Katika zoezi la vinywaji, baadhi ya waalikwa walikunywa hadi kulewa chakari na hivyo kuleta burudani nyingine.


Kwa upande wake, Rose alisema: “Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na leo naanza kurejesha furaha yangu na kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu, kwani siku chache zilizopita nilikuwa siko poa, ila leo nafurahi na ndugu na marafiki zangu kwenye siku yangu muhimu, najua pati hii imekuwa safi na hakuna aliyeboreka maana mambo yote yako vyema kabisa.”
GPL

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sio kila wakati wanawake ndio wanaoachika tu, hata wanaume wanachika pia. kuna kuachwa na kuachana, kwa hiyo jamaa ndio kachika, au kaachwa pia

    ReplyDelete
  2. Huyo bonge aliyefungua champagne shepu mbayaa na kwapa jeusiiii. Bora angejisitiri na nguo ya heshima

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad