Mbali na maafa makubwa yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na majengo ya bunge kuchomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais aliye madarakani amegoma kuachia madaraka yake.
Blaise Compaore rais wa Burkina Faso aliyekaa madarakani kwa miaka 27 anatajwa kuwa mmoja wa marais waliokaa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi na bado anasisitiza kuwa ana miezi 12 zaidi ya kuendelea kuwepo madarakani kabla ya kukabidhi madaraka kwa rais ajaye.
Ban Ki-moon anatarajiwa kuwasili nchini siku ya leo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya machafuko hayo.
Chanzo cha machafuko hayo kinatajwa kuwa ni kitendo cha bunge kutaka kufanya mabadiliko ya katiba ambayo yangemfanya Blaise Compaore kubakia madarakani kwa kipindi kingine zaidi.
Taarifa zinasema jeshi limelazimika kuongoza nchi hiyo ili kurejesha utulivu.
Viongozi wa afrika sio watu ni mashetani, kwa nini uyo raisi ku kangamana tu. Nakutaka kubandili katiba ya inchi kwa faida yake binafsi. Iyo Inchi ni mali yake bifsi. kwa nini mwengi asiongoze mpaka yeye.
ReplyDeleteWapo kimaslahi tatizo lake, ndio maana hata nchi zao hazijitambui, yaani hawafai. wengi wakingia madalakani wanafanya Taifa ndio lake tena, udicteta, wa kungangania madaraka na kurifirisi Taifa, ufisadi, wizi, rushwa ndio mambo yanakuwa yametawala, mpaka wananchi wa kawaida wanachoshwa, na umasikini uliobobea kila kona
ReplyDelete