Chenge: Asilimia 75 ya mapendekezo ya Katiba Mpya ni ya Tume

Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge la Katiba, Andrew Chenge amesema Katiba inayopendekezwa imebeba asilimia 75 ya maudhui ya Rasimu ya iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Chenge alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha michango ya hoja za wajumbe wa Bunge hilo na kamati waliyoitoa wakati wa kuhakiki Rasimu ya Katiba hiyo.

“Bunge hili limeboresha Rasimu ya Katiba vizuri sana. Rasimu hii imebeba asilimia 75 ya maudhui ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba (Joseph) na nyie wajumbe mmeboresha kwa asilimia 25 tu,” alisema Chenge.

Chenge, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), aliwataka wajumbe na wananchi wasidanganywe na tafsiri zinazotolewa pembeni baada ya Mahakama kutoa hukumu yake.

Katika hukumu iliyotokana na kesi iliyofunguliwa na mwandishi wa habari, Saed Kubenea, Mahakama ilitamka kuwa Bunge la Katiba lina mamlaka ya kuboresha na kurekebisha rasimu ya Tume.

“Maoni ya wananchi yamezingatiwa kwa kiwango cha juu sana na matumaini ya Watanzania juu ya Katiba hii ni makubwa. Mambo yao yanayowagusa yamezingatiwa,” alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad