Stori: Richard Bukos, Dodoma
KWELI ni aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini hapa.
Aibu hiyo ilimkuta staa huyo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma ambako sukari huyo wa warembo alikuwa akifanya shoo.
Aibu yenyewe iliyompata Diamond ilisababishwa na kuzimika kwa muziki wake mara tatu katika onesho hilo na hivyo kuwafanya mashabiki kupiga kelele huku wengine wakidai pesa zao za viingilio.
Hali hiyo iliwafanya mafundi mitambo kurekebisha nyaya kwa zaidi ya dakika 20 kila pale muziki ulipozimika hali iliyosababisha watu kuzidi kupiga mayowe na kumtolea maneno ya shombo Diamond, wengine wakitishia kumpopoa kwa mawe.
Muda mfupi baada ya mitambo hiyo kurekebishwa, mashabiki walianza kuserebuka tena lakini baada ya dakika 45 muziki ulizima tena na kusababisha mayowe mengine ya mashabiki wakiendelea kusema wameliwa pesa zao.
Diamond alianza kufanya tena makamuzi ndipo maiki nazo zikaanza kukoroma ambapo alianza kuwaomba wasaidizi wake wambabidilishie lakini kila waliyompa ilikuwa ikikoroma na kuwafanya mashabiki wazidi kupandwa na hasira.
Kitendo hicho kilimfanya Diamond asimamishe onesho na kuanza kumtupia lawama muandaaji (Matei) akidai kuwa ameshindwa kuweka hata betri mpya kwenye maiki alizomuandalia wakati amewatoza mashabiki kiingilio kikubwa cha shilingi 35,000 (kawaida) na 40,000 kwa VIP.
“Haiwezekani bwana, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu, mwandaaji gani unaandaa shoo, unawachaji mashabiki kiingilio kikubwa halafu unashindwa hata kuweka betri mpya kwenye maiki?
Diamond Platnumz Apata Aibu Nyingine, Dodoma Napo Pamnukia Afanya Show na Muziki wa Kigodoro
3
October 15, 2014
Tags
SIONI KOSA LA DIAMOND HAPO KWANI WAANDAJI NDIO BOMU
ReplyDeletehuyu naye anajishusha hadhi sasa, hii ni njaaa hii wala siyo chochote, kwa msanii mkubwa kama yeye inapaswa awe makini na utayarishaji wa shoo zake, kuanzia vyombo mpaka stegi, wala siyo kukurupukia dili na kwenda kupiga shoo, ndiyo maana nasema hawa wasaniii wetu wakibongo ni shobo zao tu kwamba wako vizuri kipesa kumbe hamna kitu!! jitahidini jamani msiumbuke kijinga kama hivi!!
ReplyDeletehakucheck stage kabla kama anavyofanyaga shoo za mbele ama nini
ReplyDelete