Baada ya kukubali kunyanyashwa mara mbili mfululizo msimu uliopita na Everton, hatimaye leo Manchester United ilipata nafasi kufuta uteja wao kwa klabu hiyo ya Merseysed.
Katika mchezo uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Old Trafford umemalizika kwa Man United kufuta uteja mbele ya Everton.
Kikosi cha Louis Van Gaal kimefanikiwa kupata ushindi wa 2-1.
Angel Di Maria alifungua akaunti ya magoli katika mchezo wa leo katika dakika ya 25 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Juan Mata.
Dakika moja kabla ya mapumziko Leighton Baines alikosa mkwaju wa penati baada ya Luke Shaw kumkwatua mchezaji wa Everton.
Kipindi cha pili Everton walirudi vizuri na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia Naismith.
Baada ya goli hilo Man United wakajipanga upya na alikuwa yule yule Angel Di Maria akatoa pasi nyingine ya mwisho kwa Falcao aliyefunga goli la ushindi.
United inabidi wamshukuru kipa David De Gea kwa kazi nzuri aliyoifanya kuokoa michomo ya magoli ya wazi na hatimaye wakafanikiwa kumaliza mchezo wakiwa na ushindi wa 2-1.