Halima Mdee 'Kama Serikali Walidhani Wamenikomoa Kunilaza Segerea ni Sawa na Bure, Kwasababu Nimekula ‘bata’, Ambao Sijawahi Kula'

Wakati Mbunge wa Kawe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema (Bawacha), Halima Mdee, akiachiwa huru baada ya kulala mahabusu ya Segerea kwa siku moja, amesema kuwa alikula bata ambalo hajawahi kula maishani mwake akiwa mahabusu hiyo.

Mdee na wenzake wanane, waliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es Salaam jana baada ya kutimiza masharti ya dhamana katika kesi ya kupinga amri halali ya Jeshi la Polisi na kukusanyika isivyo halali kwa lengo la kwenda Ikulu.

Mbali na Mdee, wengine walioachiwa huru ni Rose Moshi, Renina Leafyagila, Anna Linjewile, Mwanne Kassim,  Sophia Fanuel,  Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana Mdee alisikika akisema ‘people’s na wanachama hao walisikika wakiitikia ‘power’ hali iliyosababisha vurugu kubwa na kuwalazimu askari polisi wenye sare na askari kanzu kuanza kuwatawanya kutoka kwenye viunga vya mahakama.

Hata hivyo, Mdee alisimama ndani ya gari yenye namba za usajili T152 BSR aina ya Toyota V8 ya rangi nyeusi na kuwaambia waandishi wa habari kwamba, alilala mahabusu ya Segerea kimakosa.

“Kama serikali walidhani wamenikomoa kunilaza Segerea ni sawa na bure, kwa sababu nimekula ‘bata’, ambao sijawahi kula huko mahabusu…kama tulikuwa tunachechemea, sasa tunakimbia Chadema,” alisema Mdee nje ya mahakama baada ya kupata dhamana.

Mdee alitoa kauli hiyo huku viunga vya mahakama hiyo vikiwa vimefurika watu wanaodaiwa kuwa wafuasi Chadema, wakati huo huo ulinzi mkali wa askari polisi waliokuwa na silaha za moto, mbwa na gari lenye maji ya kuwasha ukiimarishwa.

Mdee na washtakiwa wenzake walipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Janeth Kaluyenda, kwa ajili ya kusikiliza masharti ya dhamana dhidi ya kesi inayowakabili, majira ya saa 6:17 mchana.

Mapema Oktoba 7, mwaka huu, Mdee na washtakiwa wenzake, walishindwa kutimiza masharti ya dhamana, baada ya nyaraka za wadhamini kushindwa kukamilika kufanyiwa uhakiki.
Upande wa Jamhuri jana uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Bernad Kongola, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salum Mohamed, na Wakili wa Serikali, Hellen Moshi.

Kongola alidai kuwa Oktoba 4, mwaka huu, katika Mtaa wa Ufipa, uliopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, isivyo halali, washtakiwa walikiuka amri halali ya Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf, iliyowataka kutawanyika.

Ilidaiwa kuwa siku na mahali pa tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko isivyo halali kwa lengo la kuandamana kwenda Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Washtakiwa wote walikana mashitaka hayo.

Upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali.

Hakimu Kaluyenda alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana wakijidhamini kwa kusaini hati ya dhamana ya Sh. milioni moja, kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi zinazotambulika.

Hakimu Kaluyenda alisema kesi hiyo itatajwa Oktoba 21, mwaka huu.

Viunga vya mahakama jana vilifurika na wanaodaiwa kuwa wafuasi Chadema, huku ulinzi mkali wa askari polisi waliokuwa na silaha za moto, mbwa na gari lenye maji ya kuwasha ukiimarishwa.
CHANZO: NIPASHE
Tags

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Heshima kwako Kamanda Mdeee, nyie ndiyo wakombozi wa hili taifa!! tunakukubali saanaaaa dada.

    ReplyDelete
  2. BIG UP MDEE NIMETOKEA KUKUPENDA GHAFLA, NYIE NDO WATU TUNAWATAKA KUONGOZA NCHI, NA SIO CCM

    ReplyDelete
  3. Mdeee hoyeeeee tunampenda tu hatamkimfanyia vituko nandiokwanza tumehamia chadema watu kibao toka ccm,hatuwapendi ccm,tumewachoka,nandiomnatufanya tuongeze nguvu chadema natutawachagua tu chadema lazima viti vya ubunge vijae chadema.nyie ccm kaeni namabavu yenu.kwanza mfe mpungue tumewachoka ccm.

    ReplyDelete
  4. HAHAHAHAHAHAHAHAH CCM NI KAMA BAHARI HATA UJAZE PIPA 100 HAITETELEKI, MPOOOOO

    ReplyDelete
  5. Viva Mdee na wenzako,nchi inahitaji wa2 majasir kama nyinyi. Ukweli 2mechoshwa na huu udikteta wa Ccm. Tunahitaj mabadiliko na mapinduz. Pepozzzzzzzzzzzzzz

    ReplyDelete
  6. poweeeeeeeerrrrrrrrrrrr, itafika siku yao tu hayoooo majimidariii cccccmmmm, kila kitu kina mwanzo na mwishooooo, kama shujaaa wangu Bob Marley alivyosema "what goes upppp, must come downnn" or "what goes around comes around" vivaaaaa dada Mdeee

    ReplyDelete
  7. Unaesifia ccm kajambe kuleeee hapa tunamuongelea halima mdee sio vitambi mdebwedo vyenu.halima hoyeeeee

    ReplyDelete
  8. teh teh teh nicheke mie mbavu zangu eti akajambeeeeeeeeeeeeeeeeee?

    ReplyDelete
  9. Hizo sifa unazozitafuta kwa nguvu zinamwisho wake, kama ulikula bata segerea kwanini umekubali kudhaminiwa na ukatoka, ungebaki huko huko upate 'kuwasaga' wenzio vizuri....SURA MBAYAAAA, SAUTI MBAYAAAAAAA kama ametiwa loba..........SIMPENDI HUYU BIBI MPAKA BASI.....

    ReplyDelete
  10. Kama humpendi lamba ndimu! Pambafu

    ReplyDelete
  11. Mama yako sura yake ni nzuri?

    ReplyDelete
  12. Wewe mwenyewe lisura lako libaya kama Rasimu pendekezwa la Miccm.....Pyuuuuuuuu

    ReplyDelete
  13. Alambe ndimu na cment mamaeeee chadema juu kwanza hawasinziagi bungeni nahawajabweteka mavitambi kama hao ccm.mtu anatambi utafikiri mtoto anajigeuza tumboni kazi kusinzia tumewachoka mmelewa madaraka kazi kujamba tu kule kupausha viti.peoples power......

    ReplyDelete
  14. piiiiiiiiiiiiiiiiiiiipooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo power.............................am proud to be chadema in ma life...HALIMA NAKUOPENDA KUFA WEWE NI WAZIRI WANGU KABISA NATAMAN NIKUONE NIKUPE MKONO WA KHELI 2015 KTK UCHAGUZII WEWE NI MWANAMKE ANA MAKINDA MBUZI HAWEZ SIMAMA NA WEWE ASHA ROSE MIGIRO NI MAJINA YAO TUU WOTE HAO AMNA KITU UKOMBOZ KARIBUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU PIIIIIIIIIIIIIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOZ POWER.ASANTE HALIMA MDEEE

    ReplyDelete
  15. kuma mkubwa wewe kama humpendi halima hata unapoishi nahisi hupapendi unajilazimisha tuuuuuuu...unamwita msagaji kashakusaga wewe au kashamsaga mama ako au dada yako...kuma wewe fala

    ReplyDelete
  16. Pipoooooooooo!!!!!..........poweeeeeeeeeeerrrrrrrr goog halima

    ReplyDelete
  17. UZUZU NI TATIZO TZ

    ReplyDelete
  18. Kweli nimeamini kusoma had unversty co kaz ishu ni kujitambua,,yan watu mnashangilia mtu kwenda mahakaman na gerezan???? Kuna faida gani utakayo pata hapo ya kimaendeleo? Tutafute ukweli co kushangia tu alafu bas..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad