Haya yamechangia Laveda kutoka mapema Big Brother

WASHIRIKI wa Big Brother Afrika wanaotokea ukanda wa Afrika Mashariki wapo katika wakati mgumu baada ya wengi wao akiwamo Laveda wa Tanzania kutoka katika wiki za mwanzoni za mashindano hayo.

Juzi Jumapili tulimshuhudia Laveda na Alusa wa Kenya wakitoka katika mashindano hayo kwa mkupuo licha ya wiki iliyopita Esther wa Uganda na Sabina na Kenya na kuaga.

Kufuatia sakata hilo, hivi sasa Afrika Mashariki imebakiwa na washiriki wanne akiwamo Frankie na Arthur kutoka Rwanda, Idris toka Tanzania na Ellah wa Uganda.

Kinachoonekana nchi nyingine kuungana na kupiga kura dhidi ya washiriki wa Afrika Mashariki.

Hata hivyo, kosa walilolifanya Idris na Laveda kupendekeza Frankie kutoka Rwanda aingie kwenye kinyang’anyiro, limesababisha nchi hiyo wiki hii kumpigia kura Ellah kutoka Uganda na kumwacha Laveda akirudi nyumbani.

Laveda amekuwa mshiriki aliyepigiwa kura na nchi moja pekee, huku akiambulia kura chache zaidi akifuatiwa na Alusa kutoka Kenya ambaye naye kura zake hazikutosha.

Hapa bado kuna shaka iwapo Watanzania waliamua kutompigia kura za kutosha Laveda kutokana na kilichotokea katika sherehe fupi iliyofanyika wikiendi iliyopita au kuna sababu nyingine.

Hata hivyo, Laveda wiki iliyopita aliongoza kwa kupigiwa kura 11 na washiriki wenzake, wakimtaka aingie kwenye kinyang’anyiro cha kupigiwa kura.

Huenda pia hali hii iliwakatisha tamaa Watanzania na nchi nyingine kutompigia kura.

Laveda amekuwa na uraibu wa kupuliza tarumbeta mara kwa mara anapokuwa katika jumba hilo, jambo hilo lilikuwa linawakera washiriki wenzake na hata baadhi ya watazamaji.

Licha ya kwamba alianza mchezo vizuri wiki ya kwanza na kuwavutia Waafrika wengi, Laveda alitibua mwishoni baada ya kudaiwa na washiriki wenzake kwamba ni rahisi kwa mwanaume yeyote kumpata iwapo atamhitaji.

Mpaka anaondoka katika jumba hilo, Laveda alikuwa ameingia katika uhusiano wa kimapenzi na mshiriki Permithias kutoka Namibia na kuonekana mara kadhaa wakibusiana, jambo lililozidi kumweka mrembo huyu matatani.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MPUUZI TU HUYU, CHANGUDOA AKAJIUZE KWAO ASIAIBISHE TAIFA. MWANGALIE KWANZA MAVHO JUU JUU TU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad