Kwa muda mrefu hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam imekuwa ikikumbwa na kashfa mbalimbali ikiwemo rushwa, unyanyasaji wa wagonjwa, na vifo vya watoto wachanga kutokana na uzembe unaodaiwa kufanywa na wauguzi wa hospitali hiyo.
Vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikiripoti kuhusu matukio yaliyowahi kutokea katika hospitali hiyo wakiwamo baadhi ya wauguzi kudaiwa kushiriki katika dhuluma ya kumbadilisha mtoto mwanamke aliyejifungua kwa kumpa mtoto mfu.
Wakati serikali na wanaharakati wakiwa katika kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na kupunguza idadi ya kasi ya vifo vya akina mama wanaojifungua na watoto wachanga, wauguzi wanaofanya vitendo hivyo vya ukatili ni lazima wapewe adhabu ili kupunguza tatizo hilo na kulitokomeza kabisa.
Akiongea na NIPASHE Jumapili jana Mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dk. Sophinias Ngonynani, alisema : "Mwananyamala imekuwa ikikumbwa na kashfa mbalimbali ikiwamo hasa rushwa na tunajua anayetoa na kupokea rushwa wote ni wakosaji hivyo tumeliona hili tatizo na kuamua kotoa elimu kwa wauguzi pia na kwa wagonjwa mbalimbali na kutokana na hili tatizo hili limeweza kupungua na kupunguza idadi kubwa ya malalamiko haya."
Aidha kwa upande mwigine alielezea jinsi wanavyokabiliana na wauguzi ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwamo vifo vya uzembe, rushwa , na unyanyasaji wa wagonjwa.
"Tumekuwa tukitumia utaratibu wa kupokea malalamiko kisha tunafanyia uchunguzi kwa umakini baada ya kuwabaini wahusika tunawachukulia hatua mbalimbali ikiwamo kuwafukuza kazi, kumuhamisha kikazi na kupewa onyo kali,” alisema.
Alisema kutokana na takwimu za ofisi za Ustawi wa Jamii, tatizo hilo limepungua kwa asilimia 80 kwa kipindi cha mwaka jana.
“Tumweza kuwachukulia hatua hizo jumla ya waauguzi 115 hivyo tunaamini tatizo hili tutaweza kulimaliza kwa kadri muda unavyozidi kwenda,” alisema. Akielezea changamoto wanazokumbana nazo, alisema watumishi wachache, bajeti, rasilimali za kufanyia kazi na uchache wa majengo ni kati ya matatizo wanayokumbana nayo.
Hata hivyo, alisema anaamini matatizo hayo yataweza kutatuliwa na hivyo kufanya huduma afya kuwa bora kwa kila mwananchi Mkazi mmoja wa Kiwalani Bombom aliyeathirika kwa kupoteza mtoto wakati akiwa anabishana na wahudumu wa hospitali hiyo baada ya kugoma kumhudumia kwa madai kuwa hakupaswa kujifungulia hospitalini hapo.
"Kwa kweli niseme tu kwamba yaliyonifika nilipokwenda kujifungua Mwananyamala yatabaki kwenye kumbukumbu maishani mwangu" alisema, Mwanahawa Ashura.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Kiongozi bora hupimwa kwa utendaji wa anaowaongoza, kuwa na misimamo, kufanya kazi kwa weledi na wewe utathaminiwa na hata ukiomba utapewa, unapokuwa Kiongozi na hiyo idara au Taasisi unayoingoza kiwa kama Mwananyama we start to dought your proffesionalism hasa katika Uongozi, Kuwa daktari si kigezo sahihi cha kuwa Kiongozi bora, Mwananyamala kwa muda mrefu wamekuwa wakiua kwa makusudi bila kujali wananchi hasa wa kipato cha chini na hata wanaopelekwa kwa matatizo kwama ajali na dharula zingine wamefariki mno, Inabidi kama wakuu wa idar ambalimbali hapo hospitalini muwe na weledi ndio kipimo cha uongozi wako kitatambulika na kuwa na mabadiliko chanya.. Wenye kipato cha juu usidhani hakuna siku utaenda hapo mwananyamala, tuchukulie umepata ajali uko mwenyewe na raia wema wamekuokota , obvious watakupeleka hospitali za serikali, na kama huduma zenyewe ndio hizi , nakwambia utapoteza masiha, kuna kijana alifariki miezi kama miwili imepita, alipata ajali saa 3 usiku kafikishwa hospitali saa 4, ,,muhudumu kaja kuanza kumpa angalau huduma ya kwanza saa 9 usiku, jamaa alikata roho, Ebu kuweni na huruma okoeni maisha , ndio mnasema mna upungufu ila, stretch yourself at the maximum hata likitoke ujue you have tried kuliko kuchukulia kisingizio cha kukosa tools za kazi na maybe budget kwa kuua watoto na kina mama na hao wanaopata ajali, Mungu awatangulie awasaidi muwe na roho ya utu..kumbuka ukimtendea ubaya wa mwenzako itakurudia na wewe kwa upande mmoja au mwingine..amen
ReplyDeleteWala sio mwananyamara peke yao Amana pia sana tu mtu unamwambia doctor nisaidie anakwambia zaa mwenyewe hao sio watu Mimi nilipanga niwarudie nije kuwatia makofi ya nguvu nimepoteza mwanangu kwa uzembe wao
ReplyDeleteHata Amana pia hivyohivyo hawana huruma hata kidogo nilipanga nije niwatie makofi ya nguvu walitaka kuniua ila nimemkosa mtoto
ReplyDelete