Kila mmoja amekua na hofu akisikia au kukutana na mtu alietoka kwenye nchi zenye zilizoathirika kwa ugonjwa wa Ebola barani Afrika na ndio maana ubaguzi umeripotiwa katika nchi mbalimbali za Amerika, Ulaya na hata Afrika.
Ripoti mpya inasema Mwanamke mmoja wa Kenya amefia kwenye uwanja wa ndege Jomo Kenyatta Nairobi kwa tetesi kwamba alikua anaumwa Ebola au Marbug ambapo familia yake imeilaumu Serikali kwa kifo cha ndugu yao kwa kutelekezwa na wauguzi kwenye Clinic ya uwanja wa ndege waliokua na hofu ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola.
NTV Kenya wameripoti kwamba Marehemu ambae alikua mfanyabiashara aliondoka nchini Kenya na kuelekea Juba Sudan ambapo alipitia Uganda wakati mlipuko wa Marbug ulipotokea na alipowasili Juba alikua anavuja damu kwenye sehemu ya uzazi jambo lililofanya dada yake amrudishe Nairobi kwa ajili ya matibabu.
Baada ya ndege kutua tu Familia yake inasema hakuhudumiwa ipasavyo ambapo kwa muda wa dakika 120 Mama yake mzazi na rafiki yake walibaki kutazama tu hali yake ikiendelea kudorora na alikua akilalamika anaumwa kichwa na amemiss mtoto wake wa kiume.
Mama Wanjiku pamoja na rafiki yake pamoja na Marehemu waliwekwa kwenye chumba kimoja kwa zaidi ya saa tano kabla ya kuruhusiwa kuondoka ambapo Wanjiku alifariki dunia akiwa kwenye kiti cha magurudumu.
Mama mzazi na rafiki yake waliruhusiwa kuondoka kabla ya matokeo ya uchunguzi wa matibabu kutolewa, kama Marehemu alikua akiugua Ebola au Marbug basi kuachiliwa kwao kungepelekea kusambaa kwa ugonjwa huo kwa haraka….