Jack Wolper Amwangukia Mkongo na Kumuomba Msamaha

BAADA ya hivi karibuni kumchana laivu Mkurugenzi wa Mwami Foundation, raia wa Kongo, Mwami Rajabu, staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kumwangukia jamaa huyo na kumuomba msamaha.

Kikizungumza na Risasi Mchanganyiko, chanzo makini kilidai kwamba baada ya gazeti ndugu na hili kuripoti habari ya Wolper kumchana Mkongo huyo huku akidai hana hadhi ya kuwa naye, wiki iliyopita alionekana kwenye Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki jijini Dar ambako ndipo alipofikia mwanaume huyo.

Kiliendelea kueleza kwamba mwanadada huyo alifika hotelini hapo kwa ajili ya kumuomba msamaha Mkongo na alikuwa akifanya jitihada kubwa ili asamehewe kwa kumtumia mwanamuziki wa FM Academia, raia wa Kongo, Patcho Mwamba amuombee msamaha.

“Nimemuona Wolper akiwa na huyo Mkongo kwenye hoteli hiyo aliyofikia ambapo kilichompeleka ni kuomba msamaha kutokana na maneno aliyozungumza kwenye gazeti,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata habari hizo kutoka kwa chanzo, kwanza alitafutwa Patcho Mwamba aliyedaiwa kusumbuliwa na Wolper akimtaka amuombee msamaha kwa Mkongo huyo ambaye ndiye aliyemuunganisha naye ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Siyo kweli kwamba Wolper anaomba msamaha mpaka sasa, kwani ameshasamehewa na wako vizuri kabisa kwani siku ile gazeti lilipotoka tu usiku wake tulikutana na Mkongo wakayamaliza.”

Kwa upande wa Mkongo alipoulizwa kuhusiana na habari hiyo alisema ni kweli Wolper alikuwa hotelini hapo akiomba msamaha huku akisema kwamba hakuwahi kuzungumza maneno kama hayo yaliyoandikwa gazetini hivyo aliamua kumsamehe.

“Nilimsamehe na sasa sisi ni marafiki wa kawaida tu siyo kimapenzi kwa sababu mimi nina mke na watoto sita na ninamuogopa sana mke wangu halafu hapa Tanzania sijaja kutafuta wanawake bali nimekuja kwa ajili ya biashara lakini nawashangaa hawa wasanii wa kike kunipakazia kwamba mimi nina uhusiano nao.

“Ipo siku nitafunguka mengi na watakoma kumendea waume wa watu,” alisema Mkongo.
Kujibu tuhuma hizo, Wolper alisema: “Watu wanasema sana lakini hakuna anayejua mimi na Mwami tukoje, kama ni bosi wangu au ni bwana wangu. Labda kama mtu aliniona nasalimiana naye akadhani nilikuwa naomba msamaha. Hakuna kitu kama hicho.”
GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad