Jaji Warioba: Siendi Ng'o Dodoma Kwenye Makabidhiano ya Katiba

Wakati Katiba inayopendekezwa ikikabidhiwa kesho kwa Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hata akialikwa katika sherehe hizo hatahudhuria kutokana na majukumu aliyonayo kwa sasa.

Jaji Warioba alisema angependa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo pia itahudhuriwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wakuu wa mikoa, mabalozi na wageni mbalimbali, lakini kutokana na dharura aliyoipata haitawezekana.

Sherehe hiyo itafanyika mkoani Dodoma kesho na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta atakabidhi nakala ya Katiba inayopendekezwa kwa Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

Katika hafla hiyo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, wajumbe wa Bunge hilo walioshiriki mchakato huo kuanzia mwanzo mpaka mwisho watapewa vyeti.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. babu kaza buti!!!

    ReplyDelete
  2. hata asipoenda sawa tu kwani yeye kazi yake alishaifanya. tatizo kila mtu anataka lake kwenye katiba hiyo kitu ambacho hakiwezekani. unapochukia kitu fulani jua mwingine anakipenda kuliko maelezo, cha msingi tuvumiliane tu na kuheshimiana basi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ushabiki siyo dili, kinachoangaliwa ni kile kilicholengwa kwa faidaya mtanzania wa leo na kesho.
      Hao walioko madarakani leo hawatakaa milele madarakani, na wanatakiwa wajichukulie kuwa wao wapo huku tuliko wananchi wa kawaida maana siku si nyingi ndivyo itakavyokuwa. Kinachotengenezwa ni kwa ajili ya WATANZANIA WOTE, WALIO MADARAKANI NA WASIO.

      Delete
    2. njoo acha kushindana na serikali iliyo badarakani

      Delete
  3. BABUU KATAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  4. WEWE UNAJUA NI MPUUZI HIV HII BLOG YAKO INA MHAKIKI KWEL?HAENDI NG'O MAANA YAKE NI NINI NDO MAANA BLOG YAKE HAIENDELEI KENGE WW

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad