Jussa Anena - 2/3 Bunge la Katiba Imekwama Angalia Mahesabu Hapa

The game is over!
Kwa mujibu wa Samuel Sitta alivyotangaza jana, jumla ya Wabunge wote wa Bunge la Katiba = 629
Tanganyika = 419
Zanzibar = 210
2/3 ya 210 = 140
1/3 ya 210 = 70
Kwa hesabu ndogo tu hapo ni kwamba kuinyima Rasimu ya Vijisenti theluthi mbili (2/3) ya Zanzibar zilitakiwa zaidi ya kura 70 (kwa maana zikipatikana 71 itakuwa hapana 2/3 ya Zanzibar).
Sasa naomba tuhesabu pamoja. Miongoni mwa wajumbe 210 wa Bunge la Katiba wanaotoka upande wa Zanzibar:
Wawakilishi wa CUF = 33 
Wabunge wa CUF ZNZ = 25
Wabunge wa Chadema ZNZ = 4
Wana UKAWA walotoka ZNZ miongoni mwa 67 = 5
Walopiga wazi HAPANA jana = 7
Wajumbe wawili (Mwanasheria Mkuu wa SMZ Othman Masoud na mjumbe Abdalla Abbas) hawakupiga kura = 2
Jumla = 76
Kuinyima two thirds ya Zanzibar ilitakiwa anything above 70 out of 210. 
Hapa pana 76
Kwa lugha rahisi kufahamika ni kwamba Katiba inayopendekezwa haitopita maana haikupata theluthi mbili ya Zanzibar.
Hapa hatujui matokeo ya kura zilizopigwa SIRI. Pia wapo wale waliotajwa kwamba wameorodheshwa watapiga kura wakiwa nje ya Bunge Maalum. Lakini hata ukichukulia zote zitakuwa NDIO basi haziwezi kubadilisha uhalisi na ukweli wa kitakwimu uliopo hapo juu.
Kwa kifupi ni kwamba theluthi mbili ya kura za Wajumbe wote wa Bunge la Katiba wanaotoka Zanzibar HAIPO.
Sijui wale waliolazimisha kuendelea na Bunge Maalum la Katiba bila ya kupata maridhiano ya pamoja na wakapelekea kutumika mabilioni ya fedha za walipa kodi masikini wa Tanzania huku wakijua kwamba hawatopata theluthi mbili ya kura za Wabunge wote wa Zanzibar sasa watasemaje?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad