Kajala Akanusha Kumshtaki Mama Yake Wema Sepetu

Kajala Masanja amekanusha uvumi ulioandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa amefungua kesi dhidi ya mama yake mzazi na Wema Sepetu kutokana kile kilichodaiwa kutukanwa na mama huyo kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Wema mwishoni mwa mwezi uliopita. 

Kajala ambaye amesema yupo busy na kazi zake binafsi, ameiambia Bongo5 hana ugomvi wowote na Wema kama watu wanavyozusha. “Hapana sijamfungulia mashtaka yoyote Mama Wema. Siwezi kufanya kitu kama hicho mama ni mzazi, mzazi kama mzazi huwezi ukasema umrudishie kitu,” amesema. “Mzazi anaweza akakutukana akakufanyia nini lakini still atabakia kuwa mzazi. Sina ugomvi wowote na Wema, hayo mambo sasa hivi hayapo ni kazi tu.”

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NANYI UDAKU MMEZIDI MPAKA MNAKERA MNAACHA KUANDIKA MAMBO YA MAANA KUTWA KUCHA KUANDIKA HABARI ZA UZUSHI NA WAANDISHI WENU WA UCHOCHORONI OVYOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  2. safiiiii k piga kazi yaache magazeti yauze tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad